Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Arusha imevifungia
vituo 57 vya kuuza dizeli, petroli na mafuta ya taa kutokana na kutokuwa na
mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs).
Akizungumza na Kusaga News juu ya hatua hiyo Meneja wa
Mamlaka hiyo mkoani Arusha Bwana Apili Mbaruku amesema vituo hivyo vipo katika
Wilaya za Arusha mjini; Karatu; Monduli; Arumeru; Loliondo pamoja na Longido.
Ameongeza kuwa waliochelewa kufunga hizo mashine za
kielektroniki za kutoa risiti (EFDs); adhabu yao ni kati ya shilingi milioni
tatu na milioni nne.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi
wa TRA Richard Kayombo amesema
kwamba wanaendelea na kazi hiyo nchi nzima ili kuhakikisha sheria
inatekelezwa.
VITUO 57 VYA MAFUTA VYAFUNGIWA ARUSHA KWA KUKOSA MASHINE ZA EFD,s
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 15, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment