Aliyekuwa mgombea udiwani Kata ya Katanini kupitia CCM Wilaya
moshi Bwana Josephat Mushi (45)
amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kukutwa na hatia ya kutapeli Sh30
milioni kinyume na sheria
Wakili wa Serikali, Lucy Kiusa amesema mshtakiwa huyo
alikutwa na hatia baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, kuridhishwa na
ushahidi uliotolewa
Hakimu Mfawidhi, Aidan Mwilapwa amesema mshtakiwa ana haki
ya kukata rufaa endapo hajaridhika na hukumu hiyo dhidi yake
Awali, Wakili Kiusa amedai Novemba 4 2015, mshtakiwa
alimtapeli Feruli Chua Sh30 milioni kwa kumuuzia kiwanja chake wakati akijua
alikichukulia mkopo Benki ya Azania.
Mashahidi wanane kutoka upande wa Jamhuri wakiongozwa na
mlalamikaji aliyedai kuwa anafahamiana na mshtakiwa kwa miaka 10 wakiwa
wafanyabiashara, amedai alinunua kiwanja hicho bila kujua kama benki iliitoa
mkopo.
Chua amedai kutokana na uhusiano wake na mshtakiwa
alimuamini ndipo alipoamua kuchukua uamuzi wa kununua kiwanja hicho
Kutokana na maelezo hayo, Wakili Kiusa alimuuliza
swali mshtakiwa kama alishawahi kuwa na kosa kabla
Wakili huyo, aliiomba Mahakama hiyo kupanga adhabu kulingana
na vifungu vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Hata hivyo, benki ilipiga mnada kiwanja hicho na kuziba deni
ya Sh15.2 milioni iliyokuwa ikidai.
Mgombea CCM afungwa jela Moshi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 02, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment