WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais, Dkt.
John Magufuli hajawahi kutangaza ama kutoa kauli ya kufutwa kwa vyama vya siasa
nchini.
Ametoa kauli hiyo leo (Februari, 2, 2017) Bungeni mjini
Dodoma wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,
Mheshimiwa Freeman Mbowe katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.
Katika swali lake Mheshimiwa Mbowe alisema Rais Dkt. Magufuli
alinukuliwa akisema atahakikisha anafuta vyama vyama vya upinzani na ifikapo
mwaka 2020 hakuna upinzani nchini
Pia Mheshimiwa Mbowe alitaka kujua nini kauli ya Serikali
kuhusu kunyimwa dhamana kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema
ambaye anashikiliwa kwa muda miezi mitatu.
Mbali na Mheshimiwa Lema, pia kiongozi huyo alitaka kujua
kuhusiana na kufungwa kwa Mbunge wa Kilombelo, Mheshimiwa Peter Lijualikali
pamoja na madiwani sita wa chama hicho ambao wamefungwa na viongozi wengine 215
wanakabiliwa na kesi mbalimbali.
Kwanza nataka nikanushe kwamba Mheshimiwa Rais hajawahi
kutangaza kuvifuta vyama vya upinzani. Pia Watanzania wote wanajua nchi hii
inaongozwa kwa sheria, kanuni na taratibu i,” amesema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “tunajua katika
kuendesha nchi tunaendesha kwa mihimili mitatu ipo Serikali, Mahakama na Bunge
na hakuna mhimili unaoweza kuuingilia mhimili mwingine,
Pia Watanzania wote wanajua kwamba jambo lolote ambalo lipo
Mahakamani haliwezi kuzungumzwa mahali pengine popote, hivyo siwezi kutumia
nafasi hii kuzungumzia mambo yote yanayoendelea chini ya sheria na yaliyo
mahakamani,” amesema.
Wakati huo huo; Waziri Mkuu amewahakikishia Watanzania
kwamba suala la upungufu wa sukari halitatokea nchini kwa sababu viwanda vya
ndani vinaendelea kuzalisha na hadi mwishoni mwa Januari vilifikia asilimia 86
ya uzalishaji
Hadi kufikia mwishoni mwa msimu wa uzalishaji ambao ni mwezi
Machi, tunaweza kuwa tumefikia malengo na kama itajitokeza upungufu Serikali
itatafuta namna nzuri ya kupata sukari kwa kushirikiana na wenye viwanda
nchini,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge
wa Mvomero, Mheshimiwa Suleiman Sadiq aliyetaka kujua hali ya sukari ilivyo
nchini kwa sasa na hatua gani zinazochukuliwa na Serikali ili kunusuru hali ya
uhaba wa sukari isijitokeze.
MAJALIWA:SERIKALI HAIJAWAHI KUTANGAZA KUVIFUTA VYAMA VYA UPINZANI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 02, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment