RAIS John Magufuli amewataka
watumishi wa idara ya Mahakama kutanguliza maslahi ya Tanzania na wamtangulize
Mungu wanapotoa uamuzi.
Rais pia ameitaka Mahakama iwe
chanzo cha mapato ya nchi, ijitathimini na yafanyike mabadiliko.
Ametoa maagizo hayo leo jijini Dar
es Salaam wakati anahutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ikiwa
mwanzo wa mwaka mpya wa Mahakama.
“Timizeni wajibu wenu, msiogope”
amesema Rais Magufuli na kuahidi kufanyia kazi ombi la kuboresha maslahi ya
watumishi wa Mahakama.
Rais amesema, anasikia mengi kuhusu
yanayoendelea kwenye vyombo ya utoaji haki na anakerwa na kauli za ‘upelelezi
unaendelea’ hata kwenye kesi ambazo ushahidi upo dhahiri.
“Lazima niseme kwa sababu nataka Tanzania
kwanza, nataka nchi yetu iende salama…ni lazima tufanye transformation
(mabadiliko) katika utoaji haki”amesema Rais Magufuli.
Magufuli: Mahakama iwe chanzo cha mapato
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 02, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment