Cynthia: Serikali iwaokoe waliofeli kidato cha nne



Mwanafunzi bora wa kike Tanzania katika matokeo ya mitihani ya kidato nne mwaka 2016 Cynthia Mchechu ameiomba serikali kutafuta njia za kuwasadia wanafunzi waliofeli mitihani hiyo ili wasipotelee mitaani.

Akizungumza alipotembelea ofisi za Kampuni ya Magazeti ya serikali (TSN) Cynthia amesema itakuwa jambo muhimu iwapo serikali itafanya kila linalowezekana kusaidia wanafunzi waliofeli hata kwa kutoa msaada wa masomo ili wasomee taaluma mbalimbali katika vyuo.

Pia amewashauri wanafunzi walioko shule kufanya bidii zaidi katika masomo.
" Nawashauri wanafunzi wanaoendelea na masomo ya kidato cha nne kusoma kwa bidii, kutii wazazi na kumuomba Mungu ili wafauli katika mitihani yao ya mwisho, na hata wafanikiwe maisha yao." alisema Cynthia

Aidha ameomba serikali kuboresha mazingira ya kufundishia ya walimu sehemu mbalimbali nchini ili kuwavutia kufanya kazi kwa lengo la kuboresha kiwango cha elimu.

"Unakuta mwalimu kasomea mjini, kakulia mjini maisha yake yako ni mjini unampeleka sehemu hakuna umeme, unategemea atafundisha vizuri kweli, hawezi kabisa," alisisisitiza.
Matokeo ya mtihani uliofanyika Novemba, 2016 yanaonesha watahiniwa wa shule 244,762 ambayo ni asilimia 70.35 ya waliofanya mtihani walifaulu mtihani huo.

Ufaulu huo unaonesha kuongezeka kwa asilimia 2.44 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015 ambayo wanafunzi 240,996 ambao ni asilimia 67.91 waliofaulu.

Jumla ya watahiniwa 408,372 walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2016, wakiwemo wasichana 209, 456 sawa na asilimia 51.29 na wavulana 1998, 916 (asilimia 48.71).
habari leo
Cynthia: Serikali iwaokoe waliofeli kidato cha nne Cynthia: Serikali iwaokoe waliofeli kidato cha nne Reviewed by KUSAGANEWS on February 02, 2017 Rating: 5

No comments: