Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) aliwajia juu wakuu hao wakati akiuliza swali bungeni leo Februari 2, 2017 asubuhi, akimtaja Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, kama mmoja wa viongozi wanaotumia msafara wa askari wengi ambao wangeweza kutumika katika shughuli nyingine za kulinda watu na mali zao badala ya kumlinda “mtu mmoja”.
Katika majibu yake kwa Mbowe, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, aliwataka wakuu hao wa mikoa na wilaya nchini kutotumia misafara hiyo mikubwa ya askari na ving’ora wanapokuwa wakielekea au kutoka ofisini. kwa ajili ya shughuli za kawaida
Kwa mujibu wa Mwigulu, wakuu hao wanaweza kuwa na misafara ya aina hiyo wanapokuwa katika matukio ya mitaani kwa ajili ya shughuli za wananchi.
Katika swali lake, Mbowe alimtaja Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kama kielelezo cha wakuu hao wa mikoa na kudai kwamba mkuu huyo wa mkoa amekuwa na msafara wa askari tisa na ving’ora na kwa hiyo, akasisitiza ni busara zaidi askari hao wakatumika katika shughuli nyingine za kulinda wananchi na mali zao.
Katika majibu yake, Mwigulu alisema wakuu wa mikoa na hata wilaya ni wenyeviti wa kamati za ulinzi katika maeneo yao ya kazi na kwa hiyo, ni jambo la kawaida kwao kuwa na misafara ya askari wanapokuwa katika kazi za umma mitaani lakini si kutumia misafara hiyo mikubwa nyakati za kwenda au kutoka ofisini.
Mbowe apinga misafara ya ving’ora kwa wakuu wa mikoa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 02, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment