TRENI YA SHIRIKA LA RELI YA KATI TRL IMEPATA AJALI NA KUPINDUKA MKOANI BWANI



Treni ya abiria ya EXPRESS ikitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam leo January 29 2017 imepata ajali maeneo ya Ruvu ndani ya mkoa wa Pwani ikiwa ni kilometa kadhaa kabla ya kufika kwenye jiji la Dar es salaam.

Shuhuda ambaye alikua ndani ya Treni hiyo amesema Behewa zaidi ya 10 zimepinduka na watu wanaendelea kuokolewa kwa kupitia Madirishani.

Amesema Treni imepata ajali kama kilometa moja kutoka Mto Ruvu, abiria wanazidi kuokolewa na haiujulikani idadi ya waliojeruhiwa wala kufariki ni wangapi

Amesema Behewa lao ndio lilikua la mwisho kuanguka kwahiyo wao tumenusurika kiasi, majeruhi wameumia na polisi tayari wameshafika eneo la tukio.








TRENI YA SHIRIKA LA RELI YA KATI TRL IMEPATA AJALI NA KUPINDUKA MKOANI BWANI TRENI YA SHIRIKA LA RELI YA KATI TRL IMEPATA AJALI NA KUPINDUKA MKOANI BWANI Reviewed by KUSAGANEWS on January 29, 2017 Rating: 5

No comments: