Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza
kulia) akizungumza katika kikao cha maandalizi ya Bajeti 2017/2017 na mapitio
ya Bajeti 2015/2016.
|
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Arusha pamoja na wadau wengine wakifuatilia Kikao cha maandalizi na mapitio ya Bajeti |
Katibu
Tawala Msaidizi huduma za Mipango Mkoa
wa Arusha Bi. Grace Mbaruku
akiwasilisha mpango wa bajeti ya 2017/2018.
|
Katibu
Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Bi.
Susane Mnafe akiwasilisha taarifa ya changamoto za usimamizi wa Halmashauri
za Mkoa wa Arusha
|
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Arusha wameagizwa kusimamia
Halmashauri zao kujibu hoja zote zilizowasilishwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha
2015/2016 kabla ya kufika mwisho wa juma lijalo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa Kikao cha maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2017/2018
na mapitio ya bajeti ya nusu mwaka wa Fedha 2016/2017 kilichohusisha Halmashauri
zote za Mkoa wa Arusha na wataalam toka
Ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za Serikali.
Akitoa Agizo hilo Mhe. Gambo alisema “Nataka kila
Halmashauri ikamilishe ujibuji wa Hoja kwa wakati na kwa majibu sahihi sio
kufanya majibu ambayo yanaibua hoja zaidi au hayajitoshelezi na kwa Halmashauri
ambayo ilipata Hati Chafu au Hati ya Mashaka kwa mwaka uliopita ianishe
wataalamu waliopelekea Halmashauri kupata Hati hizo ili waweze kuchukuliwa
hatua Stahiki”.
Wakuu wa Wilaya mshiriki Kikamilifu kuhakikisha hoja
zinajibiwa ipasavyo na wale waliosababisha hoja hizo kwa kipindi cha nyuma
wanachukuliwa hatua ili kuleta nidhamu ili kuongeza umakini katika zoezi zima
la ujibuji wa Hoja alisema Gambo.
Aliongeza kuwa “Sitamueleza Mkuu wa Wilaya ambaye
Halmashauri yake itapata Hati Chafu au ya Mashaka kwa hesabu za mwaka ulioisha,
Mkasimamie Halmashauri zenu kwa nguvu zenu zote na katika hili sitamuonea mtu
haya”.
Katika mapitio ya Bajeti ya inayoendelea alizitaka
Halmashauri ambazo hazijatoa asilimia kumi ya mapato yao kama mikopo kwa
vikundi vya wananwake na vijana zikatoe Fedha hizo kabla ya mwisho wa Januari
ili kuweza kuinua uchumi wa makundi haya yaliyoainishwa kwa mujibu wa Sera na
Maelekezo.
“Katika hili napenda kuwapongeza Halmashauri ya Jiji la
Arusha kwa kukamilisha utoaji wa mikopo zaidi ya Mil 600 kwa robo ya kwanza naya Pili
kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 lakini halmashauri zingine zote hazijakamilisha
utoaji wa Mikopo inayotakiwa kwa kipindi cha nusu mwaka.”
Awali katika Kikao hicho akiwasilisha mapitio ya Bajeti
2015/2016 na Mpango wa Bajeti 2016/2017 Katibu Tawala Msaidizi huduma za
Mipango Bi. Grace Mbaruku alisema
Halmashauri zote zinatakiwa kuandaa Bajeti Mpya kwa kuzingatia vipaumbele
vilivyowekwa katika muongozo wa Bajeti.
Halmashauri
haitazingatia vigezo vilivyowekwa inaweza kupelekea bajeti yao kukwama katika
ngazi za juu hivyo zingatieni vigezo kama kutenga Fedha za Lishe kwa ajili ya
kutokomeza udumavu kwa Watoto alisema Bi.
Mbaruku.
Akiwasilisha Taarifa ya Changamoto zinaowakabili katika
Usimamizi wa Halmashauri Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Serikali za Mitaa Bi. Susane Mnafe aliainisha
ucheleweshaji wa uwasilishaji wa Taarifa toka Halmashauri mara zinapohitajika,
kutofuata mfumo elekezi wa uwasilishaji wa Taarifa.
Aliongeza kuwa kutokua na kanzidata ya vyanzo vya mapato
na uandaaji wa Bajeti ya Halmashauri kabla ya Sheria ndogo mpya kupitishwa
huchangia kukwamisha ukusanyaji wa mapato kwa kutumia viwango vipya.
Wakuu wa wilaya za Arusha wabebeshwa mzigo mzito.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 06, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment