Serikali mkoani Arusha
imejipanga ndani ya kipindi cha miaka miwili iwe imekomesha migogoro ya ardhi
sanjari na mivutano ya mikapa ya kiutawala kati ya wilaya moja na nyingine.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo
alisema hayo kwenye kikao cha Ardhi,Kilimo,Mifugo na Mazingira kilichowaleta
pamoja wakuu wa wilaya,Wakurugenzi na Wenyeviti wa halmashauri pamoja na
maafisa wengine kujadili kwa kina mbinu za kumaliza migogoro hiyo.
Alisema baada ya uhakiki wa mipaka
na ushauri kutolewa eneo husika lipo Kijiji au wilaya fulani kiongozi au
mwananchi atakayehamasisha uvunjifu wa amani atachukuliwa hatua kali za
kisheria.
Awali Mpima Ardhi mkoa wa
Arusha,Hamdoun Mansoor akiwasilisha taarifa ya sekta ya ardhi alisema imekua
ikitoa maelekezo ya kusimamia uendelezaji katika maeneo ya vijiji na miji kwa
kuzingatia sheri ya ardhi namba 5 ya ardhi ya vijiji na 4 ya mwaka 1999
kanuni na taratibu zake.
Alisema changamoto inayoikabili
sekta yake ni ujenzi holela unaofanyika kwa kasi kubwa katika maeneo ambayo
kisheria yametangazwa kuwa maeneo ya Mpango,ambayo hayaruhusiwi kuendelezwa
bila kupata kibali kutoka kwenye mamlaka husika.
"Serikali hujikuta ikilipa
fidia zisizo za lazima wakati wa kuendeleza miundombinu mbalimbali na inapotaka
kupeleka huduma nyingine za kijamii kwenye maeneo hayo,"alisema Manssor
Aliyataja maeneo ya umma yanayopaswa
kuhifadhiwa kuwa ni pamoja hifadhi za misitu,maeneo oevu,maeneo yenye
vilima,vyanzo vya maji,mabonde na kingo za mito.
Manssor alisema uwezo mdogo wa
halmashauri kulipa fidia umefanya maendeo mengi kutopangwa na kupimwa na hivyo
kuruhusu ukuaji wa kasi wa makazi holela katika maeneo mengi ya mkoa na wilaya
zake.
Migogoro ya mipaka ngazi ya mkoa ni
katika vijiji vya Ngabobo,Olkung'wado,Leguruki,Ngejusosia,Miririnyi
wilayani Arumeru mkoa wa Arusha na Kijiji cha Lekirimuni wilaya ya Siha
mkoa wa Kilimanjaro ambayo inasababishwa na tofauti ya matangazo ya serikali
namba 135 la mwaka 1954
MKOA WA ARUSHA KUKOMESHA MIGOGORO YA ARDHI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 08, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment