MKUU WA WILAYA YA KARATU AWASIHI WANANCHI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI AMBAVYO NI MSAADA KWA MAISHA YAO



Mkuu wa wilaya ya karatu
Mkuu wa wilaya ya Karatu Bi Theresia Mahongo amewaomba wananchi wake kutunza vyanzo vya maji kwa kuwa wakifanya hivyo watakuwa wanatunza pia uhai wa maisha yao.
Amesema kuwa katika wilaya hiyo kuna chem chem ya maji iitwayo kusmayu ambayo inahudumia vijiji sita na imekuwa msaada mkubwa lakini kuna baadhi ya watu ambao hawapendi kutii shera wamekuwa wakiharibu chanzo hicho cha maji.

Bi Theresia amesema kuwa mwezi wa nane alitembelea eneo la chemchem hiyo na kukuta baadhi ya wananchi wamelima vitunguu na Mazao mengine lakini kwa kuwa hawakuwa wanafahamu kuwa ni kosa akawapa muda watakapovuna mazao hayo wasilime tena awamu nyingine lakini baadhi yao wakakaidi.

Kufuatia hatua hiyo Bi theresia akafanya ziara katika eneo hilo la chem chem na kukuta baadhi yao wamevunja maagizo ambayo ametoa miezi kadhaa iliyopita kwamba wasilime karibu na chanzo hicho na kuamua kuwachukulia hatua kwa kuwakamata watu 14 ambao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Amesema watu hao waliokamatwa 6 wanatoka kijiji cha kurus na watu wengine 8 kutoka kijiji cha kusmayu ambapo walikutwa wanalima karibia na vyanzo vya maji na walishakatazwa kufanya hivyo.

Pamoja na hayo Bi theresia ameleza kuwa lengo hasa ni kutunza vyanzo vya maji ambavyo ndiyo vinavyotegemewa katika matumizi ya binadamu na kusema kuwa hakuna mtu atakayeonea mtu lakini endapo akivunja sheria lazima zisimamiwe kwa weledi kwa kushirikiana na wananchi.

Vile vile amewataka wananchi kuendelea kuhamasishana kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kupanda miti ili kuendelea kutunza mazingira yanayozunguka vyanzo vya maji kwa kuwa Bila maji hakuna maisha na maji ni uhai.
MKUU WA WILAYA YA KARATU AWASIHI WANANCHI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI AMBAVYO NI MSAADA KWA MAISHA YAO MKUU WA WILAYA YA KARATU AWASIHI WANANCHI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI AMBAVYO NI MSAADA KWA MAISHA YAO Reviewed by KUSAGANEWS on January 08, 2017 Rating: 5

No comments: