Busara itumike katika matumizi ya maji ya bonde la Eyasi


Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa kikao cha viongozi wa dini pamoja na wazee wa Karatu.
Katika Kikao kingine Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho  Gambo(aliyesimama mbele) akizungumza na Wazee wa Karatu pamoja na Viongozi wa Dini.
 
Mtaalamu wa Halmashauri ya Karatu(kwanza kulia) akiwaandikisha  Wananchi wa Kijiji cha Oldeani waliojiunga na Mfuko wa afya ya Jamii wakati wa Mkutano wa hadhara na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na walimu wa Wilaya ya Karatu wakati wa ziara yake ya Kikazi Wilayani humo.

Serikali Mkoani Arusha imesema busara ilipaswa kutumika zaidi katika Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa alilotoa wakati wa ziara yake Wilayani Karatu katika Bonde la Eyasi kuhusu kusogezwa kwa Mashine za kuvuta maji Umbali wa Mita 500 kutoka chanzo cha Maji.

Katika Agizo lake Mhe. Waziri Mkuu aliagiza kusogezwa kwa mashine za za kuvuta maji kutoka chanzo cha maji cha bonde la Eyasi ambapo akati mchakato wa utekelezaji ukiendelea baadhi ya wakazi wa eneo hilo walizichoma moto mashine hizo ambazo kwa wakati huo zilikuwa zimesogezwa umbali wa mita 60 ambazo zinaruhusiwa kisheria.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani Karatu amesema kutokana na umuhimu wa bonde la Eyasi katika uzalishaji wa Chakula haikuwa busara kwa wananchikuchoma mashine hizo bila kujali mazao ambayo tayari yameshaoteshwa katika eneo hilo na gharama zilizotumika kununua mashine hizo.

Aliongeza kuwa wananchi hao walienda mbali zaidi kwa kujichukulia sheria mikononi na kuharibu mali mbalimbali ikiwemo nyumba za wamiliki wa mashine hizo hali iliyopeleka kuleta hofu, usumbufu na sintofahamu kwa wananchi wa maeneo hayo.

“Vyombo vya ulizni na usalama vupo kwanini wananchi hawa wasiende kuripoti tatizo hilo kwenye vyombo vinavyohusika na badala yake wanaamua kujichukulia sheria Mkononi, Kisheria hairuhusiwi kwa mtu yeyeote kuharibu mali ya mwananchi ilikua ni lazima tuwachukulie hatua wote waliofaya uharibifu ule” Alisema Gambo.

Mhe. Gambo aliongeza kuwa haikuwa rahisi kwa wananchi wa Mang’ola kuamua kufanya zoezi lile pekeyao inaonekana kuna viongozi wa Kisiasa ambao wako nyuma ya vurugu zile na sisi kama Serikali tunaamini jukumu la kiongozi ni kuleta Amani na sio uvunjifu wa Amani na ukienda kinyume sheria inafuata mkondo wake.

“Hivyo katika kudhibiti vurugu zile wananchi wote na viongozi wao waliohusika kwa namna moja ama nyingine kufanya uharibifu wa mashine na mali za wananchi tuliwakamata na kuwapeleka Mahakama ili iwe fundisho katika maeneo mengine” Alisem Gambo.

Kwa kuwa sasa wahusika wamekwisha tambua makosa yao tunaweza kukaa pamoja na kuangalia namna gani bora ya kutumia maji ya bodne hili bila kusababisha vurugu za aina yeyote ili kila mtuamiji aweze kunufaika na maji ya bonde hilo.

Bonde hilo linatumiwa na wananchi zaidi ya elf 20 wanaojishughulisha na shughuli za Kilimo cha mazao mbalimbali kwa njia ya umwagiliaji hutegemea maji yanayotoka katika Bonde la Eyasi .
Busara itumike katika matumizi ya maji ya bonde la Eyasi Busara itumike katika matumizi ya maji ya bonde la  Eyasi Reviewed by KUSAGANEWS on January 10, 2017 Rating: 5

No comments: