Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi na
kupotosha wananchi kwa kuwa vinahatarisha amani ya nchini.
Rais Magufuli ametoa onyo hilo wakati akikagua na kufungua
Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga
Rais Magufuli amesema Serikali haitayavumilia magazeti hayo
mawili kwa kuandika habari za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya
nchi kama ilivyotokea katika nchini ya Rwanda na kupelekea mauaji ya kimbari
nchini humo.
Serikali ya kutumbua majipu haiwezi kuacha kutumbua magazeti
yanayofanya mambo ya uchochezi hatuwezi kuiacha Tanzania ikawa dampo la eneo la
kuweka maneno ya uchochezi chini ya utawala wangu hilo halitakuwepo kuna
magazeti mawili tu kila ukisoma wao ni kuchochea tu ikizungumzwa habari hii wao
wanageuza hii nasema na nataka wanisikie siku zao zimeshafika kama wanasikia
wasikie wasiposikia wasisikie lakini magazeti mengine na vyombo vyote vingine
vinatoa uchambuzi mzuri sana
Rais Magufuli amesema Serikali yake haiwezi kuvumilia kuona
amani ya nchi inahatarishwa na magazeti mawili kwani amani ndio chimbuko la
maendeleo ya taifa lolote duniani.
Amesema bila kuwepo kwa amani hakuna mwekezaji atakayeweza
kuja kuwekeza nchi, hata wawekezaji wa ndani watashindwa na hivyo kurudisha
nyuma maendeleo ya nchi.
Rais Magufuli amesema uwepo wa amani nchini ndio uliowezesha
wawekezaji wa Kiwanda cha Fresho cha kutengenezea mifuko ya kubebea bidhaa za
chakula nchini na kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani
Shinyanga kujengwa mkoani hapo kwani bila amani visingeweza kujengwa.
Aidha ameitaka Benki ya Uwekezaji Nchini TIB na Taasisi
nyingine za fedha kutoa mikopo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika viwanda
badala ya kuwakopesha wanasiasa ambao hutumia fedha wanazokopa kwa matumizi
yasiyowanufaisha watanzania waliowengi
Rais Magufuli ameupongeza uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa
kuanza kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya kutaka Tanzania ya viwanda
kwa kujenga viwanda vingi mkoani humo ikiwa ni pamoja na viwanda hivyo viwili
alivyovizindua katika siku yake ya mwisho ya ziara mkoani Shinyanga.
Rais Magufuli Atoa ONYO Kali Kwa Magazeti
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 14, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment