KICHANGA CHAFARIKI BAADA YA KUKEKETWA.



MTOTO mchanga amefariki Dunia kutokana na kuvuja damu nyingi, baada ya kukeketwa akiwa na umri wa siku tano.

Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha, kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, alilsema lilitokea katika kijiji cha Naibera, wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.

Kamanda alisema uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha kuwa kichanga hicho kilizaliwa Siku ya Krismasi, Desemba 25, 2016 na kwamba Desemba 30, 2016, majira ya saa nne asubuhi, Bibi yake alimchukua na kumkeketa

Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa  baada ya mtoto huyo kukeketwa, hali yake ilibadilika na kuwa mbaya kutokana na kutokwa na damu nyingi na ndipo alipokimbizwa hospitali ya rufaa ya k KCMC iliyoko mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

“Baada ya mama wa mtoto huyo aitwae Fatina Joshua, (14), kuona damu inazidi kumtoka mwanae na hali yake inakuwa mbaya, aliamua kumkimbiza katika Hospitali ya KCMC Januari 11, 2017,kwa ajili ya matibabu”, alisema kamanda Mutafungwa.

Aliendelea kusema kuwa baada ya kupokelewa hospitalini hapo, madaktari waligundua kuwa sehemu zake za siri zilikuwa zimeharibiwa vibaya kutokana na kukeketwa ambapo alifariki Dunia Januari 13, 2017.

Kamanda alisema Baada ya kupata taarifa za kifo cha mtoto huyo kutoka KCMC, Jeshi la polisi lilianza uchunguzi ili kubaini chanzo chake na ndipo walipogundua kuwa alikeketwa.
Aidha kamanda alisema kufuatia tukio hilo,Jeshi la polisi limemkamata Bibi huyo aitwae Longida Naingola pamoja na mama wa mtoto aliefariki Dunia kwa uchunguzi zaidi.

Alisema polisi mkoani humo kwa ushirikiano na jeshi la polisi mkoani Manyara kulikotokea tukio hilo, wameanza msako mkali wenye lengo la kukomesha vitendo vya ukeketaji ambavyo vinaonekana kushamiri katika Mkoa wa Manyara.




KICHANGA CHAFARIKI BAADA YA KUKEKETWA.  KICHANGA CHAFARIKI BAADA YA KUKEKETWA. Reviewed by KUSAGANEWS on January 14, 2017 Rating: 5

No comments: