Serikali haina mpango wa kugawa chakula- RC Gambo

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo amefunguka na kusema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haipo tayari kumletea chakula mwananchi ambaye alishindwa kukitunza chakula alichovuna. 

Mrisho Gambo amesema hayo alipokuwa Wilayani Karatu mkoani Arusha katika ziara yake ya siku tano na kusisitiza kuwa serikali inachoweza kufanya ni kutoa elimu kuhusu kilimo bora kupitia wataalamu wake.

"Serikali kwa ufupi haina mpango wa kumletea chakula mtu ambaye anachakula chake amekivuna na ameshindwa kukutunza vizuri, ameshindwa kujiwekea akiba harafu anategemea serikali itangaze hali ya hatari, nachoweza kusema kazi yetu sisi ya kwanza ni kuja kuwaelimisha juu ya kilimo bora kupitia wataalamu wetu". Alisema Mrisho Gambo 
Serikali haina mpango wa kugawa chakula- RC Gambo Serikali haina mpango wa kugawa chakula- RC Gambo Reviewed by KUSAGANEWS on January 14, 2017 Rating: 5

No comments: