CCM NA CHADEMA WATWANGANA MAKONDE MKOANI MOROGORO



VURUGU baina ya wafuasi wa chama cha Demokarsia na Maendeleo CHADEMA na chama cha mapinduzi CCM zimeibuka mara baada ya kampeni za udiwani zinazoendelea mjini Morogoro na kusababaisha watu wanne kujeruhiwa maeneo mbalimbali ya miili yao.

Vurugu hizo zilizohusha aina mbalimbali ya silaha mawe fimbo na mapanga zilitokea majira saa 1 eneo la Lukwngule karibu na ofisi za chama cha mapinduzi CCM baada ya maandamano waliyofanya wafuasi wa vyama hivyo kugongeana hapo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya mashuhuda wa vurugu hizo Pili Hosen na Rajabu Kimario walisema vurugu hizo ziliibuka baada wafuasi wa CCM kukutana eneo moja na wafuasia wa chama Chadema kisha kuanza kusrushiana maneno mali kisha kuanza kurushiana mawe.
 
“CCM wakiawa na gari lao la matangazo wakipiga nyimbo zao za hamasa walikuja hadi hadi hapa(Lukwangule) wakati huo huo Chadema nao wakiwa na wafuasi wao na gari lao la matangazo ya hamasa akakutana hapa…ukatokea mzozo kwa muda mfupi baadae wakaanza kurushiana mawe kwa karibu nususaa hivi”alisema Pili.

Katibu wa siasa,itikadi na uenezi CCM Wilaya ya Morogoro Maulidi Chambilila mbali na kukili kuibuka kwa vurugu hilo watu wanne walijeruhiwa akiwemo Lukoo Chingwi aliyepasuliwa na jiwe kichwani,Tausi Saidi aliyejeruhiwa mbavuni kwa jiwe na fimbo,Gelard Jeilaikaialiyechomwa kisu mbavuni na Kurwa Hanu aliyejeruhiwa kisogoni kwa jiwe.

“dhamira ya chama ni kumaliza uchaguzi huu kwa amani na atakaeshinda hata kama ni kutoka upinzani aendelee na shuguli zake kwa amani sio tumalize uchaguzi na majeruhi ambao mwisho wasiku ni doa ndani ya vyama vyetu…tunaliomba jeshi la polisi kuwa makini na usalama hususani kipindi hinki cha kuelekea kwenye uchaguzi”aalisisitiza Chambilila.

Kwa upande wake katibu mwenezi wa Chadema Morogoro Shabani Dimoso alisema chama hicho na wafuasi wake walikutana na msafara huo wakirudi kutoka kwenye kampeni eneo la Kimunyu na walipofika eneo hilo walianza kushambuliwa kwa mawe na matusi jambo lililowatawanya na kusambaratika ovyo.

“unajua wenzetu ni watu wa kutumia dola sana, juzi(jana)wakati tukitoka kwenye kampeni tulikutana na wenzetu wa CCM eneo la Lukwngule hapo ndiopo ikazuka vurugu na kuanza kurushiwa mawe jambo lilowasambaratisha wafuasi wetu bila hata hatia yoyote…lakini hata hivyo wakaita na polisi lakini hawakukuta mtu”alisema Dimoso.

Alieongeza kuwa  hata hivyo wakiwa ofisini kwao tawi la Kiwanja cha ndege majira ya asubuhi polisi walikwenda na kumkamata mwanachama  wao Ratifa Malumbu  waliyefanikiwa kumdhamini jana.

Kamnda wa polisi mkoa Urlichi Matei amekili kutokea kwa tukio hilo nakuwa ni watu wawili walioripotiwa polisi kujeruhiwa huku akiahidi kuimarisha ulinzi ikiwemo kukomesha aina zote za maandamano baada ya mikutano hiyo ya kampeni.

“sina taarifa kamili ya wanaoshikiliwa juu ya tukio hilo isipokuwa kuna watu wawili walijeruhiwa na kuripotiwa kwetu na niongeze tu kuwa tumeimarisha ulinzi kwenye mikuta hiyo ya kampeni ikiwemo kuanzaia sasa ni marufuku kuwepo kwa mandamano yoyote mara baadaa ya kampeni hizi zinazoendelea”alifafanua kamanda Matei.

Kampeni za uchaguzi mdogo nchini zinahusisha jimbo moja la uchaguzi Zanzibar na kata 24 nchini kote ambapo mkoani Morogoro ni kata moja ya Kiwanja cha ndege inayotaraji kufanyiwa uchaguzi wa Diwani baada aliyekuwa diwani wake Godfrey Mkondya kufariki dunia


CCM NA CHADEMA WATWANGANA MAKONDE MKOANI MOROGORO CCM NA CHADEMA WATWANGANA MAKONDE MKOANI MOROGORO Reviewed by KUSAGANEWS on January 14, 2017 Rating: 5

No comments: