KAMPENI za udiwani kata
ya Kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro zimeingia katika hatu nyingine baada
ya jeshi la polisi mkoani hapa kulivulumishia milipuko inayosadikiwa kuwa
mabomu ya machozi gari la matangazo la chama cha cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA kisha kupora kompyuta mpakatoa iliyokuwa ikitumika mkurusha matangazo
na kutoweka nayo.
Tukio hilo lililojiri
jana(januari 13)kuanzia saa 12.30 hadi saa 1.15 jioni mara baada ya mkutano wa
kampeni katika mtaa wa Lutogo mjini humo lilisababisha wakazi wa mitaa jirani
kujificha majumbani kwa muda huku wengine akiwemo Paulina Samweli(27)
kujeruhiwa mguu huo na milipuko hiyo.
“mimi nilikuwa napita
zangu kwenda Msamvu mara tukasikia mlio wa bomu sijui kama ni risasi au nini
tukageuza kukimbia,muda kidogo mbele akatokea polisi ameshika bunduki na
kufyatua kutuelekezea sisi…ukafumuka moshi mwingi miguuni ndio imenibabua hivi
mguu wangu wa kulia”alisema Paulina.
Mbunge wa viti maalumu
mkoani Morogoro Devotha Minja akiwa ameshika mabaki ya maganda yaliyosadikiwa
kuwa ya Mabomu ya machozi alisema kuwa mwendelezo wa serikali ya chama cha
Mapinduzi CCM kukandamiza demokrasi kupitia vyombo vya dola hasa jeshi la
polisi unaendelea.
“watanzania ni mashuhuda
jinsi serikali ya CCM inavyotumia vyombo vya dola kuminya demokrasia nchini
kama ambavyo leo imedhihilika jinsi polisi wanavyotumika hata kukiuka makusudi
sheria na kanuni za uchaguzi”Alisema Devotha na kuongeza.
“kitendo cha kuzuia
Chadema kuwajuza wananchi kesho kitakuwa wapi na kamapeni zake huku CCM
ikiachwa kuendelea na matangazo ya aina hiyo hiyo ni ubaguzi zaidi wa rangi
wala ukabila”Alisema Devotha.
Devotha alisema wakati
kampeni hizo zipo kati kati jeshi la polisi limeanza kutumika na ccm kudhofisha
upinzani kwa kuwabebesha makosa mbalimbali likiwemo la shambulio,matumizi ya
silaha na kuzuia kujinadi kwa uhuru mbele ya wapiga kura ambao Januari 26
wanataraji kufanya maamuzi ya mwisho kwa kumchagua wanaeona anawafaa.
Mwenyekiti wa baraza la
wazazi chadema manispaa hiyo Omary Mvwambo na mratibu wa uchaguzi huo Innocent
Zawadi waliitaka tume ya uchaguzi kukaa na jeshi la polisi mkoani morogoro
kulielekeza mifumo ya usimamizi wa usalama kwenye mikutano na baada ya kampeni
majukwaani.
Kwa upande wake
mwanasheria wa Chadema Bathromeo Tarimo alionyesha kushangazwa na nguvu
inayotumika na jeshi la polisi dhiidi ya wafuasi wa chama hicho akiobainisha
kuwa hali ilivyo ni kama kunaupinzani kati jeshi la polisi na chadema.
“nilisihi jeshi hili
hasa kumwelekeza kamanda wa polisi mkoa kufanyua kazi kwa weledi likizingatia
sheria,kanuni na taratibu zinazotawala tukio kwa kipindi hicho badala ya
kuvamia vamia na kupiga mabomu katika mazingira yenye mchanganyiko wa watu…sasa
imekuwa kama ligi kati ya chadema na polisi basi wavue magawanda waje
tushindane majukwaani”alishauri Tarimo
Mwanasheria Tarimo
alisema mtindo wa jeshi la polisi kuacha kazi yake ya kulinda usalama wa raia
na malizao na kuwa sehemu ya washindani katika kinyang’anyilo cha ugombea kisha
kutumia mamlaka yake kupora vifaa vya chama kimoja nikosa lisilo faa huku
akilitaka jeshi polisi kujirekebisha mapema.
Akizungumzia hali hiyo
Kamanda wa polisi mkoani hapa Urlich Matei alikili jeshi hilo kuwapiga mabomu
wafuasi wa Chadema ingawa alikana kutowajeruhi watu na kuwa wamenyakua Kompyuta
mpakato wanayoishikilia huku akiwataka wafuasi hao kufuata makubaliano
waliyoafikiana kutofanya maanadamano wala mikusanyiko isiyo na tija baada
ya muda wa kampeni.
“watalalama sana
wanapaswa kubadirika, wanakuwa kama watoto wasio na maadili bwana! Hapa leo
tumeongea na kutahadharisha kuwa kuanzia sasa haturuhusu maandamano wala
mikusanyiko baada ya muda wa kampeni lakini wao wanatumia sijui kiburi ndi
wanaenda kufan ya hay ohayo”alisema kamanda Matei.
Alisema jeshi hilo
limejidhatiti kwa nguvu zote kuimarisha usalama wa raia na malizao nakuwa
haliko tayari kusikia mtanzania yeyote anabugudhiwa au kudhalilishwa dhii ya
lolote hususani kipindi hiki cha uchaguzi.
CHADEMA WAFURUSHWA KWA MABOMU YA MACHOZI KWENYE KAMPENI UDIWANI MOROGORO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 14, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment