Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha) |
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Pamoja na
Jeshi la Polisi mkoani hapa kufanikiwa kuongeza takwimu za ukamataji wa madawa
ya kulevya kwa makosa 75 zaidi kwa mwaka 2016 kulinganisha na mwaka
2015,imeonekana kwamba mwaka huu 2017 kwa kushirikiana na vyombo
vingine vya Usalama pamoja na Tume ya Kuratibu na Kudhibiti dawa za kulevya
nchini, kasi hiyo ya kuthibiti kilimo cha madawa ya kulevya aina ya bhangi
ambacho kinalimwa baadhi ya maeneo ya wilaya ya Arumeru imeanza mapema.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisi kwake mara baada ya operesheni ya kutokomeza
madawa hayo kufanyika kwa siku mbili, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu
Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba Jeshi hilo pamoja na vyombo
vingine limeamua kuanza kuharibu mimea iliyopo mashambani mapema hasa kipindi
hiki cha masika ambapo uoteshaji ufanyika ili kazi ya kudhibiti madawa hayo
huko mbeleni iwe rahisi.
Kamanda
Mkumbo alisema katika operesheni hiyo jumla ya hekari 31 za mimea ya bhangi
ziliharibiwa huku gunia 58 na kilogramu 210 ziliteketezwa kwa moto katika
maeneo ya kijiji cha Kismiri Juu kata ya Uwiro tarafa ya King’ori na katika
kijiji cha Engalaon kata ya Mwandeti tarafa ya Muklati wilayani Arumeru.
“Siku ya
kwanza Jumanne tarehe 10.01.2017 Operesheni hiyo ilifanyika katika kijiji cha
Kismiri Juu kata ya Uwiro tarafa ya King’ori na kupata jumla ya magunia 31 ya
bhangi na kilogramu 210 za mbegu zilipatikana huku hekari 19 za mimea hiyo
ziliharibiwa”.
“Siku ya
tarehe 12.01.2017 Alhamisi operesheni hiyo iliendelea tena katika maeneo ya
kijiji cha Engalaon kata ya Mwandeti tarafa ya Muklati na kufanikiwa kupatikana
kwa magunia 27 na kuharibu hekari 12 za mimea ya bhangi hivyo kufanya jumla ya
magunia 58 kupatikana, mbegu kilogramu 210 kupatikana na hekari 31 za mimea huo
kuharibiwa”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.
Kamanda
Mkumbo alitoa onyo kali kwa viongozi wanaoishi au kufanyia kazi maeneo hayo,
kuacha mara moja kuwaunga mkono wakulima wa bhangi.
“Jeshi la
Polisi mkoani hapa linawaonya viongozi wa maeneo ambayo zao hilo linalimwa
kuacha mara moja kuwaunga mkono wakulima hao, naamini ulimaji mpaka uuzaji wa
bhangi unafanywa kwa uwazi katika maeneo hayo bila wao kuchukua hatua”.
“Watambue
kwamba wao ni walinzi wa amani katika maeneo yao na washirikiane na Jeshi la
Polisi katika kutokomeza kabisa kilimo hicho cha bhangi ambayo inaleta madhara
makubwa kwa jamii hasa kundi la vijana”. Alisisitiza Kamanda Mkumbo.
Naye mkuu
wa kitengo wa kuthibiti dawa za kulevya nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Jeshi la Polisi(SACP) Mihayo Msikhela alisema Jeshi la Polisi nchini
limejipanga hasa kwenye kuzuia kuliko kutibu ndio maana wameamua kuharibu
mapema mimea ya zao hilo haramu kabla ya kukomaa na kusambaa.
Alisema
kwamba kiwango cha uteketezaji wa dawa za kulevya hapa nchini kwa mwaka 2016
kiliongezeka ikilinganishwa na mwaka juzi 2015.
Kwa upande
wake Afisa sheria mkuu toka Tume ya Kuratibu na Kuthibiti dawa za kulevya Bi.
Christina Gervas alisema kwamba kadri bajeti itakaporuhusu watazidi
kushirikiana na vyombo vya Usalama kufanya operesheni mara kwa mara katika
maeneo ambayo bhangi inalimwa na pia kuahidi kutoa elimu kwa wakulima na
viongozi wa maeneo hayo ili waweze kuachana na zao hilo haramu na kujikita
kwenye mazao halali ya chakula na biashara.
MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA YAZIDI KUSHIKA KASI KISIMIRI JUU WILAYANI ARUMERU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 14, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment