Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mtu mmoja kwa
tuhuma za kufukua kaburi la marehemu ambaye likuwa ni mlemavu wa ngozi aliyefariki
mwaka 2010 kwa lengo la kuchukua viungo vyake.
Inadaiwa kuwa marehemu alifariki dunia mwaka 2010 kwa ugonjwa wa homa na kuzikwa katika makaburi ya Kijiji cha Mumba.
Mtuhumiwa alikutwa na majembe na makoleo ambayo walikuwa wakiyatumia kufukuria kaburi hilo. Baada ya mahojiano mtuhumwa huyo aliwataja washirika wenzake wawili ambao walikimbia baada ya kuwaona askari.
Jeshi hilo linaendelea na msako mkali wakuwatafuta watuhumiwa unaendelea.
Katika tukio lingine Mnamo tarehe 03.01.2017 majira ya saa 3:30 usiku katika kata ya Makongolosi wilayani Chunya, mkoa wa Mbeya, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la KELVIN KUBANDA mkazi wa Kahama alikamatwa akiwa na bhangi kete 10 sawa na uzito wa gramu 55.
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa katika kijiwe cha kuvutia Bhangi. Upelelezi unaendelea.
Anaswa na polisi akifukua kaburi la albino Aliyefariki tangu mwaka 2010
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 04, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment