|
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo
akikabidhi hundi ya Tsh Mil 199 kwa wawakilishi wa Vijana Amos Kosani (Daraja II) na
Janeth Prosper (Kata ya Unga Ltd).
|
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro(Kwanza
kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mhe. Mrisho Gambo kukuabidhi hundi kwa vikundi vya Wanawake na Vijana wa
Jiji la Arusha.
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo
amefungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vinavyokopeshwa na kutoa mikopo
kwa vikundi 85 vya wanawake na vikundi 40 vya vijana kutoka katika kata zote za
Jiji la Arusha.
Akikabidhi hundi zenye thamani ya Sh Mil 624 kwa
vikundi hivyo ikiwa ni mikopo ya robo ya kwanza na ya pili kwa mwaka wa fedha
2016/2017 Mhe. Gambo amewataka kinamama na vijana kutumia
fedha hizo kwa shughuli zilizokusudiwa ili ziweze kuleta manufaa na kuwatoa
katika lindi la umasikini.
“Mikopo hii
inatolewa ili kuendeleza shughuli za kijasiriamali ambazo ndizo zilizopelekea
mkidhi vigezo vya kupata Fedha; Nimatumaini yangu fedha hizi zitawawezesha
kuongeza mitaji yenu na kuwapa ari ya kujituma zaidi huku mkizingatia nidhamu
ya pesa ili muweze kuzirejesha kwa wakati na makundi mengine waweze kupata
fedha hizo”Alisema Rc Gambo.
Aliongeza kuwa tofauti na mikopo hii ya halmashauri baada
ya kuwawezesha vijana waendesha boda boda kwa kuwapatia Pikipiki 200 kundi
litakalofuata ni wakinamama ambao watanufaika na Fedha zitakazorejeshwa na
vijana hao kwa kupewa mitaji midogomidogo kadiri ya uhitaji.
Aidha Rc Gambo alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji kuunda
timu maalumu ya kuchunguza utoaji wa Mikopo kwa Kipindi cha Miaka mitatu kama
ilifuata taratibu, vikundi vilivyonufaika kama ni hai na hali ya urejeshaji.
Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti
Lazaro Bukhay ambaye alishiriki katika zoezi la utoaji mafunzo na kukabidhi hundi amesema
Kikundi ambacho hakitarejesha fedha zote za mkopo ama kuchelewesha marejesho
kwa namna yeyote ile hakitapatiwa mkopo katika mwaka unaofuata ila wale
watakaofanya vizuri katika biashara zao na kukuza mitaji wataongezewa kiasi cha
kukopa kulingana na hali ya shughuli zao.
Mikopo hiyo inayotolewa kwa mujibu wa Sheria na
miongozo inayoelekeza asilimia kumi ya
Mapato ya ndani ya Halmashauri kutolewe kama Mikopo ya riba nafuu kwa vikundi
vya wananwake na vijana na kwa jiji la
Arusha kiasi kinachotakiwa kutolewa ni Bil 1.2 kwa Mwaka huu wa Fedha hivyo
kiasi kilichotolewa ni kwa kipindi cha nusu mwaka.
Fedha hizo
zinatolewe kwenye Saccos au Vicoba vyenye nguvu katika Kata husika ili
kurahisisha usimamizi na urejeshaji wa mikopo hiyo. Hivyo Saccos na Vicoba
ndizo zinazokopesha vikundi vilivyoainishwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata
(WDC) kwa riba ya asilimia 10 na wao hubaki na asilimia 8 kwa ajili ya shughuli
za uendeshaji na kurejesha Halmashauri riba ya asilimia 2 tu.
Rc Gambo akabidhi Tsh. Mil 624 Kama Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake na Vijana
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 03, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment