Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akifungua kikao cha
Wadau wa Elimu Mkoa wa Arusha
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo akishirikiana na wataalamu kuweka mitambo sawa kwa ajili ya
wadau wa Elimu kuwasilisha taarifa.
|
Viongozi wa Halmashauri ya Ngorongoro wakifuatilia Kikao cha Wadau
wa Elimu
|
Wadau wa Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
|
Kaimu Afisa Elimu Mkoa Ndg. Emmanuel Mahondo akiwasilisha taarifa ya Elimu Mkoa wakati wa Kikao cha wadau wa Elimu kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha |
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amewataka wadau wa elimu kuunganisha
nguvu zao katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ili kufikia
malengo ya Serikali ya ufaulu wa asilimia 80 kila wilaya.
Gambo ametoa wito huo katika kikao chake na Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi wa Halmashauri ,Maafisa Elimu wa Shule za Sekondari na Msingi
pamoja na wadau wengine wa Elimu mkoani hapa.
Alisema ili kufikia malengo ya Matokeo Makubwa Sasa(BRN)
yanayotaka ufaulu katika ngazi ya Elimu ya Msingi na Sekondari kufikia asilimia
80 lazima kuwepo na vifaa vinavyohusika kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia.
“Katika kuangalia elimu kwa mapana yake, hatuna budi
kuwajengea uwezo walimu wetu kwa kuwapa mafunzo ya mara kwa mara ili kuwapa
motisha badala ya kuwaacha na elimu waliyoipata Chuoni pekee,” alisema Gambo
Pia aliagiza Halmashauri zote za Mkoa huu kununua
Mashine za kufyatulia matofali tambazo zinapatikana kwa gharama nafuu kutoka
shirika la viwanda vidogo (Sido) ili kurahisisha zoezi la ufyatuaji wa matofali
kwa matumizi ya Shule.
Aliwataka Wakuu wa Wilaya Mkoani hapa kuona namna
wanavyoweza kuwashirikisha wananchi kuchangia nguvu zao katika kufyatua
matofali mara baada ya halmashauri kukamilisha ununuzi wa mashine za kufanyia
kazi hiyo toka Sido.
“Uchakavu wa majengo na upungufu wa vyumba vya madarasa
pamoja na vyoo imekua ni changamoto ya muda mrefu katika Sekta ya Elimu lakini
viongozi mkifanikiwa kuwahamasisha wananchi kuchangia nguvu kazi katika miradi
ya Elimu itasaidia kukarabati na kukamilisha ujenzi wa miundombinu kwa wakati
muafaka hivyo kuboresha upatikanaji wa Elimu bora kwa watoto wetu”.
Naye kaimu Afisa Elimu mkoa wa Arusha, Emmanuel Mahondo amesema hali ya elimu
imekua ikiimarika kwa ufaulu kuongezeka na kuwa katika mkoa wa Arusha ni
halmashauri za Arusha Jiji na Arusha DC ndizo zilifikia viwango BRN.
Kikao hiki na wadau wa Elimu ni muendelezo wa vikao vya
Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na wadau
wa sekta mbalimbali katika Mkoa huu kujadili changamoto na kuona namna ya
kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja.
RC Gambo akutana na wadau wa Elimu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 03, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment