Mhandi wa Maji Happy Mrisho
(aliyesimama) akiwasilisha taarifa
ya mradi kwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha(hayupo pichani) wakati wa kikao cha kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Maji Makilenga.
|
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Makilenga waliohudhuiria kwenye
Mkutano wa hadhara.
|
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.
Alaxander Mnyeti akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga kwenye
Mkutano wa hadara.
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Nkoasenga kwenye Mkutano wa hadhara
|
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga wakifurahia makubaliano yaliyofikiwa katika ya Serikali na kijiji hicho ya kulipa Tsh 1500 kwa huduma ya maji mwezi mzima kwa wanaotumia mabomba ya Kijiji |
Nteghenjwa Hosseah - Arumeru
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe .
Mrisho Mashaka Gambo amemaliza mgogoro wa muda mrefu uliodumu zaidi ya
miaka mitatu kati ya Bodi ya Maji ya Makilenga na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga,
Kata ya Leburuki Wilayani Arumeru.
Utatuzi wa mgogoro huo
ulifikiwa kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Nkoasenga
baada ya Mhe. Gambo kuwashirkisha
wananchi wa aneo hilo katika kutatua changamoto hii iliyoathiri wananchi zaidi
ya hamsini elfu wa kijiji hiki pamoja na vijiji vingine ishirini na sita
vinavyotegemea mradi huo.
Wananchi hawa waliofungiwa
maji kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa baada ya kufanya uharibifu wa miundombinu ya
Maji pamoja na kuweka kinyesi kwenye mabomba walionyesha kuchoshwa na adha hiyo
ya kufuata maji umbali mrefu na kwa gharama kubwa zaidi ilihali maji
yanapatikana katika Kijiji chao na walionyesha hali ya kutaka muafaka wa jambo
hili ili kuendelea kupata huduma ya maji kama ilivyokuwa hapo awali.
Akiongea katika Mkutano huo
baada ya mazungumzo na viongozi wa Kijiji pamoja wananchi Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo alisema katika kutoa huduma
ya Maji Vijijini tunaongozwa na Sera ya Maji ya mwaka 2002 inayotaka kuchangia
hudma za maji na sio kununu Maji hivyo kila kaya inawajibu wa kuchangia kiasi
kidogo cha Fedha ili kuwezesha huduma hii iendelee kutolewa siku zote.
“Tunafahamu kwamba
maji haya yanaanzia kwenye Kijiji hiki
na wakazi wa Nkoasenga ndio walinzi
wakuu wa mradi huu na wanastahili kupewa
upendeleo wapekee katika kutumia maji
haya ili wendelee kutunza mradi huu wa
Maji, ni wazi kuwa vijiji vya ukanda wa
chini haviwezi kupata Maji endapo tu wana Nkoasenga wataharibu mradi huu wa
maji mtiririko”, Alisema Mhe. Gambo.
Aliongeza kuwa umuhimu huu wa
nyie kuwa Kijiji mama cha mradi huu hauwapi Kinga ya kutokuchangia gharama za maji, hivyo nataka
mniambia mnaweza kuchangia kiasi gani kadiri ya uwezo wenu na baada ya
makubalino haya mtalipia gharama za maji
kwa mwezi na sio kwa mwaka tena kama mlivyokuwa mnafanya
hapo awali”.
Awali akizungumza katika
Mkutano huo Mhandisi wa Maji Bi. Happy
Mrisho alisema “mradi wa maji Makilenga uliibuliwa na wananchi wa Kijiji
cha Nkoasenga na baada ya thatmini ya
awali ilonekana kuwa mradi ni wa gharama kubwa hivyo usingekidhi vigezo vya
kiufadhili kama ungekua mradi wa kijiji kimoja na ili kukidhi vigezo vya kupata
fedha toka kwa wafadhili ililazimu kuongeza wanufaika kutoka vijiji 26 na
utekelezaji ukaendelea”.
Aliongeza kuwa baada ya
mradi kukamilika iliundwa Kamati tendaji ya Makilema ambayo ndiyo inayosimamia
mrdai huu na Madiwani na wenyeviti wote wa vijiji waliingia makubaliano ya kuchangia
Tsh 10 kwa ndoo lakini baada ya muda mfupi wanakijiji wa Nkoasenga
walikiuka makubalino hayo na kudai watalipa Tsh 5000 kwa mwaka na hawewezi
kulipa kwa ndoo kwa kuwa maji hayo ni mali
ya Kijiji.
Anderson
Sikawa ni Diwani wa Kata ya Leburuki kilipo kijiji cha
Nkoasenga alisema hawakatai kuchangia huduma za Maji lakini kutokana na hali
duni ya wananchi wa eneo hilo hawawezi kulipa kwa ndoo hivyo wanahitaji kufanya
mapitio ya gharama za Maji ili kuendana na hali ya wana Nkoasenga ambayo pia
itawaongezea ari wakazi hao kulinda mradi huo kwa manufaa ya vijiji vingine pia
alitoa tuhuma kwa Bodi ya Makilenga kwa
matumizi mabaya ya Fedha za maji.
Katika kutoa mapendekezo ya
kiasi stahiki cha kuchangia huduma ya Maji Ndg.
Afred Masao ambaye ni mwananchi wa Kijiji cha Nkoasenga aliwakilisha
wananchi wote wa Kijiji hicho alisema kuwa
wananchi wako tayari kuchangia
kwa mwezi lakini uwezo wao ni Tsh 1500 na
sio Ths 3000 kama ilivyopendekezwa kwenye vikao vya ndani katika ya Mkuu wa
Mkoa na viongozi wa Kijiji.
Rc
Gambo alihitimisha Mkutano huo kwa kukubaliana na mapendekezo
ya wananchi kuwa watalipia Tsh 1500 kwa mwezi kwa wale wanaotumia mabomba ya
Kijiji na kwa wale wenye mabomba nyumbani watalipia kadiri ya matumizi yao kwa mwezi na wote watafungiwa Mita za Maji pia aliwaagiza wananchi hao kulipia gharama hizo
Halmashauri na sio kwa Kamati ya Maji Makilenga kama awali.
Mradi wa Maji wa Makilenga
ulianza mwaka 2011 kwa lengo la kutoa huduma ya Maji na kuhudmia Kata nne na vijiji 27; Ulifadhiliwa na
Jumuiya ya Ulaya kwa kutoa kiasi cha Tsh Bil 3.7, OIKOS pamoja na nguvu za
wananchi. Mradi huu unaendeshwa na Jumuiya ya watumiaji maji ya Makilenga
ambayo ina jukumu na mamlaka ya Kisheria kusimamia mradi huu wa maji.
MKUU WA MKOA AMALIZA MGOGORO WA MAJI - MAKILENGA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 10, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment