RC Makonda atembelea Uwanja wa Fisi wanapofanya biashara ya ngono....Aahidi Kupavunja na Kujenga Viwanda Vidogovidogo
Jumapili Novemba 27 Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda aliendelea na ziara yake katika maeneo mbalimbali
ya jiji la Dar es Salaam akiwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi na
kuzitatua.
Akiwa katika ziara hiyo, Mkuu wa
Mkoa alipita katika viunga vya Kata ya Manzese na kutokea sehemu ambapo kula
kilabu kinachouza pombe za kienyeji huku watu waliokuwa eneo hilo wakionekana
kuwa wamelewa kiasi cha kutotambuana.
“Hii achana nayo kabisa ni moto wa
kuotea mbali. Hebu niikate kidogo uone,” Mzee
aliyefahamika kwa jina la Mandela alisikika akimtambia Paul Makonda huku
akipiga funda la pomne hiyo ya kienyeji hali inayoonyesha kuwa hakuwa akifahamu
kuwa anayezungumza naye ni Mkuu wa Mkoa.
Baadaye alienda eneo lenye vibanda
vya chumba kimoja kimoja, amabavyo inaelezwa kuwa ni madanguro ambayo hutumika
kufanyika biashara ya ukahaba hadi kwa wasichana wenye umri mdogo. Hata hivyo
kila mlango aliojaribu kugonga ulikuwa umefungwa na hakuna aliyeitika na
kufungua mlango.
“Hawa wakijua watu wa serikali
wanakuja hapa basi hufunga biashara zote, sasa na hapa wamefunga, si rahisi
kumpata mtu,” alisikika kijana mmoja mwenyeji wa
eneo hilo akisema.
Akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Tandale, Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alisema
serikali inafanya mipango ya kupata wawekezaji ili kununua eneo hilo la Uwanja
wa Fisi na kuwalipa fidia wakazi wa eneo hilo ili vibanda vyote vivunjwe na
kujengwa vitegauchumi badala ya kuliacha eneo hilo liharibu maisha ya vijana.
RC Makonda atembelea Uwanja wa Fisi wanapofanya biashara ya ngono....Aahidi Kupavunja na Kujenga Viwanda Vidogovidogo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 28, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment