Godbless Lema Akwama Tena Mahakamani Baada Ya Mawakili wa Serikali Kuweka Pingamizi .........Amerudishwa Rumande Hadi Disemba 2
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema leo amefikishwa tena Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa ajili ya kusikiliza
rufaa yake ya maombi ya dhamana.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa
mahakamani hapo huku wafuasi wa Lema wakiwa wamevaa fulana nyeupe
zilizoandikwa Jutice 4 Lema mbele zikiwa na picha yake.
Mbele ya Jaji Fatma Masengi
aliyekuwa amepangwa kusikiliza Rufaa hiyo, Upande wa Jamhuri ambao
ulikuwa ukiwakilishwa na mwanasheria Matenus J Marandu umeweka pingamizi kwamba
mawakili wa Lema walipaswa kupeleka notisi ya rufaa kwanza na siyo kukata rufaa
Wakili wa Chadema Peter Kibatala
amesema wao wameshakamilisha taratibu zote za kisheria, hivyo wanasubiri uamuzi
wa pingamizi hilo lililowekwa na upande wa serikali.
Jaji Fatma Masengi ameutaka
upande wa serikali uwasilishe hoja za pingamizi lao kwa njia ya maandishi
kabla ya November 30 ili aweze kutolea uamuzi December 2 mwaka huu.
Godbless Lema Akwama Tena Mahakamani Baada Ya Mawakili wa Serikali Kuweka Pingamizi .........Amerudishwa Rumande Hadi Disemba 2
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 28, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment