Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti wa serikali ya
Mtaa wa Zavala kata ya Buyuni Ilala, Chiku Said baada ya kutuhumiwa kuuza
viwanja vya watu pamoja na serikali kinyume na sheria.
Hatua hiyo imekuja baada ya
wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kuuza viwanja vya serikali
kinyume na sheria bila kuwahusisha wajumbe wenzake hali ambayo imesababisha
mgogoro mkubwa wa ardhi katika eneo hilo.
Hatua hiyo ilimfanya mkuu wa mkoa huyo kumtaka Afisa Ardhi wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela kuthibitishwa kuuzwa kwa eneo hilo kinyume na sheria.
“Mkuu wa mkoa, ni kweli tulikuwa na eneo Block J lakini limeuzwa,” alisema afisa huyo “Nataka kuwaambia kitu mwenyeviti wa mtaa hawaruhusiwi kuuza eneo katika mtaa. Mimi ningewataka wenyekiti kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa ili kuepuka kutokea kwa hayo mambo,”
Baada ya kauli hizo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameliliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
RUNGU LA RC MAKONDA LAMUANGUKIA M/KITI MTAA WA ZAVALA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 24, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment