Siku nne baada ya rais John Pombe Magufuli kuivunja bodi ya
mamlaka ya mapato Tanzana ametaja sababu iliyomsukuma kuchukua uamuzi huo.
Rais John Pombe Magufuli ameweka bayana sababu hiyo wakati
akihutubia hadhara ya mahafali ya 31 ya chuo kikuu huria Bungo Kibaha mkoani
Pwani kuwa ni kuchukuwa fedha za serikali na kuziweka katika fixed account kwa
nia ya kujipatia fidia.
Rais Magufuli pia amemwagiza waziri wa elimu sayansi na
teknolojia Prof Joyce Ndalichako kuchukua hatua kwa viongozi wa mamlaka ya
elimu nchini tea kwa kuweka fedha katika fixed account fedha walizopaswa
kuzitumia ktk kutatua changamoto ya madarasa na mabweni.
Pia rais amemtaka waziri wa elimu Pof Joyce Ndalichako
kuhakikisha anasimamia kiwango na ubora wa elimu kwa wanafunzi wanaodahiliwa
ktk vyuo vikuu nchini kwa kuzingatia viwango vinavyohitajika vya kujiunga na
elimu ya juu ili kusimamia ubora na viwango vya wahitimu.
Aidha waziri wa elimu Joyce Ndalichako amekataa ombi la
makamu mkuu wa chuo hicho aliyetaka uwepo wa upendeleo kwa viwango vya udahili
kwa wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho.
RAISI MAGUFULI ATAJA SABABU ZILIZOMSUKUMA KUVUNJA BODI YA TRA NCHINI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 24, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment