Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka kiwanda cha Mt. Meru Miller mjini Arusha. |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na uongozi wa kiwanda cha Mt. Meru Millers mara baada ya kufanya ziara kiwandani hapo. |
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali
inajipanga kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye viwanda kama
hatua ya kuviwezesha viwanda vingi nchini kuongeza uzalishaji na kutoa
ajira nyingi kwa
watanzania.
watanzania.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha baada ya
kutembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Mount Meru Millers ili
kujua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho ili Serikali iweze kuzifanyia
kazi katika kuleta unafuu kwenye uzalishaji wa mafuta ya kupikia nchini.
Makamu wa
Rais amesema mlolongo wa kodi zinazotozwa kwa wamiliki wa viwanda hazina
uratibu mzuri hivyo mkakati ya Serikali wa awamu ya Tano inataka kuweka
utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo ikiwemo kuondoa kodi ambazo ni kero
kwenye viwanda.
Amesisitiza
kuwa Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha viwanda vingi vinajengwa
nchini ambavyo vitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini hali ambayo
itasaidia uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kuuzwa kwenye masoko ya
nje ya nchi na kuliingizia taifa mapato na kuongeza ajira kwa makundi
mbalimbali ya wananchi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ziara ambazo anafanya kwenye viwanda mkoani
Arusha ni kujionea jinsi viwanda hivyo vinavyofanya kazi za uzalishaji na pale
kwenye changamoto zinazokwamisha viwanda hivyo kufanya kazi vizuri ziweze
kufanyia kazi na Serikali.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mount Meru Millers Atul Mittal amesema
kama Serikali itafuta au kuondoa utitiri wa kodi wanazotozwa kwenye Viwanda
hivyo watakuwa na uwezo wa kuongeza maradufu uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa
Watanzania.
Amesema
kwa sasa Kampuni hiyo inafanya kazi kwenye nchi 10 barani Afrika na kwa
Tanzania pekee imeajiri wafanyakazi zaidi ya 1000 ambao wanafanyakazi katika
maeneo mbalimbali nchini.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ATEMBELEA KIWANDA CHA MT. MERU MILLERS KILICHOPO NJIIRO MKOANI ARUSHA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 24, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment