Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeunda tume
kuchunguza taarifa inayoelezea utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka
Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye
Hifadhi ya Grumeti Serengeti pamoja na kutafuta kaburi la faru huyo.
Amesema timu hiyo ya wataalamu tayari imeshafika Sasakwa VIP
Grumet kwa ajili ya kutafuta kaburi na kuchukua vinasaba vya masalia ya faru
John na kisha watakwenda kwenye Hifadhi ya Ngorongoro kuchukua vinasaba vya
watoto wake na kuvilinganisha na pembe
hiyo ili kubaini kama kweli pembe
aliyopelekewa ni ya faru John au laa.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kikazi
mkoani Arusha iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kuona
utoaji wa huduma kwa wananchi.
Amesema wakati faru John akiwa V I P Grumet taarifa zilisema ni mgonjwa na daktari alipompima mara
ya kwanza akabaini faru huyo hakuna na ugonjwa wowote; kisha alimpima tena kwa mara
ya pili taarifa zikasema tena si mgonjwa
ghafla wakasema amekufa jambo ambalo amesema haliwezekani.
Waziri Mkuu ameiagiza timu hiyo kufanya kazi ya uchunguzi wa
taarifa hizo kikamilifu kwa sababu Serikali imetumia fedha nyingi kuwaleta faru
hao kutoka nchini Afrika Kusini hivyo ni lazima nyara hizo za Serikali zilindwe
kwa manufaa Taifa.
BADO VINA SABA ILI TUTAMBUE KWELI PEMBE ILIYOLETWA NI YA FARU JOHN
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 18, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment