MKUU WA WILAYA YA KARATU AENDELEA KUTEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU ALIYOTOA WAKATI WA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA
Mkuu wa wilaya ya karau Theresia mahongo akiwa na mkuu wa mkoa wa arusha mrisho gambo |
Kufuatia agizo la Waziri Mkuu kasimu majaliwa kuagiza wale wote wanaotumia pampu za umwagiliaji kwenye chanzo cha maji katika maeneo ya mang'ola wilayani karatu wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo husika.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu sa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo amesema kuwa tayari wameshatekeleza agizo hilo ambapo jumla ya pampu zilizokuwa kwenye vyanzo vya maji zilikuwa 26 ampabo pampu 21 wananchi wenyewe walizitoa.
Bi Theresia amesema kuwa wananchi wenye pampu 5 walikaidi na kupelekea kuwakamata na kuwapeleka polisi ambapo wanategemea kufikishwa mahakamani kutokana na kuharibu vyanzo vya maji.
Ameongeza kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia ya kubaribu vyanzo vya maji ambavyo vinategemewa na jamii kwa ajili ya kuwasaidia katika umwagiliaji pamoja na matumizi mengine hivyo kama serikali hawatavumilia MTU mmoja kutumika ili kuweka hasara kwa wengine.
Pamoja na hayo amewataka wananchi kutii sheria na taratibu kwa kuwa wilaya ta Karatu ni kwa ajili ya wananchi wote na kama serikali hawataonea mtu Bali watafuata sheria zinavyosema ili haki kutendeka kwa pande zote.
MKUU WA WILAYA YA KARATU AENDELEA KUTEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU ALIYOTOA WAKATI WA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 18, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment