Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg.
Athumani Kihamia(mbele) akishiriki kuchimba Msingi wakati wa uzinduzi wa
ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet.
|
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.
Gabriel Fabian Daqarro(mbele) akizungumza na wananchi wa Kata ya
Muriet(hawapo Pichani) wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet.
|
Wananchi wa Kata ya Muriet wakishiriki katika Ujenzi wa Msingi wa
Kituo cha Afya, zoezi la ujenzi limezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro.
|
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg.
Athumani Kihamia akihamasisha
wananchi kuendelea kuchangia nguvu kazi katika ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet
wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Kituo hicho.
|
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.
Gabriel Fabian Daqarro akishirkiana na wananchi kuchimba Msingi kwa ajili
ya ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet.
|
Wakazi zaidi ya 27,000 wa kata ya
Murriet iliyopo Jiji la Arusha wataondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa
zaidi ya km 15 kusaka huduma ya Afya na kujifungua kwa akina mama baada ya Mkuu
wa wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro kuzindua ujenzi wa Kituo cha Afya
kitakachogharimu zaidi ya shilingi milioni 400 katika kata hiyo.
Kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha
Afya kitakachokuwa cha kisasa ni kufuatia malalamiko ya muda mrefu ya wananchi
wa eneo hilo kwa Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa alipokuwa katika ziara Mkoani
Arusha hususani katika Jiji la Arusha kuwa kata hiyo yenye wakazi hao haina
zahanati wala kituo cha afya cha uhakika na kufikia hatua ya akina mama
kujifungulia nyumbani au njiani wakati wakienda katika kituo cha Afya za
Levolosi kilichopo umbali wa km 15 .
Kufuatia malalamiko hayo ya
akina mama waliokuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali ya kutaka kituo cha
afya au zahanati,Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza mara moja huduma hiyo kuwafikia
wananchi bila ya kuchelewa.
Mhe. Daqarro alisema kuanza kwa
ujenzi wa kituo hicho ni kufuatia jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mhe. Mrisho
Gambo kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi kama vile matofali 3, 000, mifuko ya sementi
100 na bati 100 kwa ajili ya ujenzi huo.
Alisema na kuwataka Halmashauri ya Jiji kwa kushirikiana na wananchi wa kata hiyo kufanya kila
linalowezekana kuhakikisha Kituo hicho cha Afya hiyo kinakuwa na maabara, chumba cha Upasuaji pamoja chumba cha wagonjwa
wa nje sambamba na vifaa vya kisasa ili wananchi waliokuwa katika kata hiyo kupata
huduma na kuondokana na adha ya kusafiri umbali mrefu.
Naye Mkurugunezi wa Jiji Ndg.
Athumani Kihamia alisema Rais Dkt. John
Magufuli katika kipindi cha kampeni aliahidi kila kata kote nchini kuwa na
zahanati au kituo cha afya cha uhakika kwa ajili ya kusongeza huduma ya
afya kwa wananchi hivyo Jiji la Arusha limeanza kutekeleza Ahadi hiyo .
Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dr.
Bakari Salumu alisema kuwa Jiji la Arusha linaupungufu wa vituo vya Afya 9 na
zahanati 11 kwani vilivyopo havikithi mahitaji ya wananchi kwa sasa.
Dr. Bakari aliongeza kuwa kwa sasa Jiji la Arusha lina zahanati 71 na
vituo vya afya 16 mahitaji ambayo bado hayakithi matwaka ya wakazi wa Jiji hilo
lenye mitaa 154 ambalo linakuwa siku hadi siku.
Alisema Kituo hicho cha Afya
kinachojengwa kitakuwa na vifaa vyote muhimu na madaktari wa kutosha kutoa
huduma hiyo kwani kata hiyo ndio yenye wakazi wengi kuliko kata yoyote katika
Jiji la Arusha.
Huduma za Afya kusogezwa kwa wananchi wa Muriet -Arusha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 20, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment