WIZARA YALAANI VIKALI UKEKETAJI WA WATOTO WA KIKE KATA YA KIVULE, MANISPAA YA ILALA, JIJINI DAR ES SALAAM
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakemea vikali
vitendo vya ukeketaji vinavyotaarifiwa kufanyika katika Kata ya Kivule, Manispaa
ya Ilala jijini Dar es salaam, na mikoa mengine ambayo imekaririwa na vyombo
vya habari.
Wizara inaagiza wazazi na walezi kuacha mara moja vitendo vya ukeketaji
kwani ni ukatili, husababisha madhara kwa watoto wa kike na wasichana ni kosa
la jinai.
Athari za ukeketaji kwa wahanga ni pamoja na kusababisha
majeraha kwa watoto, vifo, vilema, maradhi kama fistula na mengineyo. Watoto wa kike na wanawake wamekuwa wakifanyiwa
ukatili wa vitendo vya ukeketaji bila ridhaa yao na wakati mwingine ridhaa hiyo
huwa imepatikana kwa hila, jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
Wizara inatoa rai kwa vyombo vya dola kuwakamata wazazi, walezi, mangariba,
na wote wanaoendeleza vitendo vya ukeketaji dhidi
ya watoto wa kike na wasichana katika kata ya Kivule na maeneo mengine nchini, na kuwafikisha mahakamani ili sheria iwezekuchukua mkondo wake.
Wizara
itaendelea kupambana na vitendo vya ukeketaji vinavyotaarifiwa katika jamii
zetu, na itaongeza juhudi ya utoaji elimu kwa jamii sambamba na kuwachukulia
hatua wote wanaojihusisha na mila potofu ya ukeketaji.
Wito
unatolewa kwa kila mwananchi kushiriki katika kuzuia vitendo vya ukeketaji na
hasa kufichua matukio ya ukeketaji, na kutoa ushahidi mahakamani ili wahusika
waweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Wizara
inatoa rai kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii katika
Mikoa, Halmashauri na Kata katika maeneo ambako kunaarifiwa kuwepo vitendo vya ukeketaji
kuhakikisha kuwa wanashirikiana na mamlaka husika kuzuia ukatili huo katika
nchi yetu.
WIZARA YALAANI VIKALI UKEKETAJI WA WATOTO WA KIKE KATA YA KIVULE, MANISPAA YA ILALA, JIJINI DAR ES SALAAM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 20, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment