Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema),
Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu jana aliwaomba radhi wakazi wa Mbeya,
wanafamilia, ndugu wa marehemu Recho Lutumo (14) aliyefariki dunia baada ya
kugongwa na gari lake juzi.
Ajali hiyo ilitokea wakati gari hilo
lililokuwa likiendeshwa na Gabriel Andrew (43) mbunge huyo akiwamo lilipokuwa
likitoka jijini hapa kwenda Uwanja wa Ndege Songwe (Sia).
Recho ambaye ni yatima na aliyekuwa
akilelewa na bibi yake Neema Lutumo, aligongwa wakati akivuka kwenye alama za
watembea kwa miguu eneo la Iyunga katika barabara kuu ya Zambia.
Sugu akiwa na baadhi ya viongozi wa
Chadema jijini Mbeya alishiriki maandalizi na shughuli zote za mazishi ya mtoto
huyo kuanzia nyumbani ambako ndiko alikoomba radhi.
Sugu Awaomba RADHI Wakazi wa Jiji la Mbeya Baada ya Gari Yake Kuua Mtoto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 19, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment