Wanafunzi wa kike 12 wanaosoma Shule
ya Msingi Nditi, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, wamekumbwa na ugonjwa wa
kuanguka ghafla na wengine kupoteza fahamu, walipokuwa wakicheza katika viwanja
vya shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Amon
Livigha, alikiri kutokea tukio hilo katikati ya wiki iliyopita, saa mbili
asubuhi.
Alisema baada ya tukio hilo, baadhi
ya wazazi walifika shuleni hapo na kuwachukua watoto wao na kwenda nao
nyumbani.
“Nilipata taarifa ya kuanguka kwa
wanafunzi hao nikiwa darasani nafundisha, hivyo kutokana na uzito wa tatizo,
nililazimika kukatisha masomo na kwenda kuwahudumia watoto hao.
“Wakati tukiendelea kufanya
utaratibu wa kuwakimbiza wanafunzi hao kituo cha afya kupatiwa huduma, baadhi
ya wazazi walikataa watoto wao wasipelekwe hospitali na kuondoka nao,” alisema.
Mwalimu Livigha alisema kutokana na
tukio hilo, kamati ya shule, wazazi na uongozi wa Serikali ya kijiji na kata
hiyo wamekutana kujadili suala hilo.
Mtendaji wa kata hiyo, Juma
Mng’anga, alikiri kutokea tukio hilo na kueleza kuwa tayari wameshatoa taarifa
makao makuu ya wilaya, Nachingwea.
Wanafunzi wakumbwa na ugonjwa wa kuanguka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 15, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment