WANDISHI WAFUKUZWA KWA MITUTU NA ASKARI MAGEREZA WAKIWA KATIKA MAJUKUMU YAO MAHAKAMANI ARUSHA

Waandishi wa habari wametishiwa kupigwa risasi na askari magereza kwenye viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa arusha waliofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutimiza majukumu yao ikiwemo kuandika habari inayomkabili mbunge wa arusha mjini.

Wandishi hao waliokuwa wamefika mahakamani hao saa mbili na dakika 28 na basi la magereza lilipofika wandishi hao walitoa camera zao kwa ajili ya kupiga Lema picha lakini gafla askari zaidi ya 6 walishuka kwenye basi hilo wakiwa na silaha za moto na kuanza kuwakimbiza huku wakiwatolea lugha za vitisho licha ya kuwa na vitambulisho vya kazi na kibali cha mahakama cha kupiga picha.

Wandishi hao Lilian Joel wa Gazeti la uhuru,Emanuel kalemba wa star TV,zulfa mussa wa Gazeti la Mwananchi,Veronica Ignatius, na Janeth Mushi wa Gazeti la mtanzania, walikimbizwa na askari hao wa magereza wakiwa na silaha huku waandishi hao wakijitetea kuwa ni waandishi lakini hawakusikilizwa.

Hata hivyo waandishi hao walilazimika kukimbia na ndipo wakakutana na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Nestory Baro ili awaokoe kwa kuwa alikuwa amesimama nje karibu na chumba cha mahakama na kulazimika kuwatetea ili kujiokoa kwa kuwa askari hao walikuwa wanawakimbiza.

Hakimu nestory alisikitishwa na kitendo hicho cha askari hao kuwakimbiza waandishi ambao walifika mahakamani muda wa saa 8:28 asubuhi kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili Mbunge wa arusha mjini Godbless.
Kwa mara ya kwanza lema kuletwa Kwa ajili ya kesi mbili za uchochezi namba 440 na 441 polisi kwa kushirikiana na askari magereza waliwafukuza wandishi wa habari na kuwakataza kuingia kwenye chumba cha mahakama kwa ajili ya kusikiliza kesi ya mbunge huyo.

Jana waandishi walifukuzwa mahakamani Hapo baada ya Askari hao kuwataka watu wote watoke nje ya mahakama na kuwafukuza mpaka nje ya geti wakiwa wanawatishia huku wakiwa wamebeba silaha za moto ambapo kitendo cha askari hao kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za mahakama.

Baada ya hapo waandishi wakamua kutoa taarifa kwa hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Agustino Rwizire kuhusu kitendo cha askari hao ambapo aliwaomba radhi na kuahidi kuandika barua kwenda kwa RPC na Mkuu wa magereza.

Lakini pia amesema kuwa askari magereza hao wataendelea kuingilia majukumu ya wandishi atawaomba mamlaka husika kuwabadilisha ili waletwe Askari wengine kwa kuwa mahakama ni mhimili unaojitegemea.

Tangu Mbunge huyo ameanza kuletwa mahakamani hapo askari magereza kwa kushirikiana na askari polisi wamekuwa wakifukuza na kuwakataza wasihudhurie mahakamani hapo.
WANDISHI WAFUKUZWA KWA MITUTU NA ASKARI MAGEREZA WAKIWA KATIKA MAJUKUMU YAO MAHAKAMANI ARUSHA WANDISHI WAFUKUZWA KWA MITUTU NA ASKARI MAGEREZA WAKIWA KATIKA MAJUKUMU YAO  MAHAKAMANI  ARUSHA Reviewed by KUSAGANEWS on November 16, 2016 Rating: 5

No comments: