POLISI mkoani Dodoma inawashikilia
walimu watatu wa shule za sekondari kwa tuhuma ya kuwazuia wanafunzi wa kidato
cha nne, kufanya Mtihani wa Taifa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,
Lazaro Mambosasa alisema kwamba walimu hao wa shule za sekondari za Zoissa na
Mnyakongo wilayani Kongwa, walikamatwa Novemba Mosi mwaka huu.
Kamanda Mambosasa alisema kwamba,
wakati wa mtihani wa somo la Kiingereza, walimu hao walimzuia mwanafunzi Amina
Said wa shule ya sekondari Zoissa kwa madai ya kuwa ni mjamzito na kumpeleka
kituo cha afya, kupimwa muda wa mtihani, lakini majibu yalionesha hakuwa na
ujauzito.
Aidha, mwanafunzi Bahati Ntigonza wa
shule ya sekondari Mnyakongo, alizuiliwa kuingia katika chumba cha mtihani kwa
kuwa hakuvaa sare ya viatu, hivyo alirudishwa nyumbani kuvaa viatu huku wenzake
wakiendelea na mtihani.
Kamanda Mambosasa aliwataja
watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Lukonge Mwezo ambaye ni Mkuu wa Shule ya
Sekondari Mnyakongo, Omari Athumani Mkuu wa Shule ya Sekondari Zoissa na Daud
Suleimani John aliyekuwa mwalimu wa zamu katika shule ya sekondari Mnyakongo.
Walimu Watatu Watiwa Mbaroni Kwa Kuwazuia Wanafunzi Kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 04, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 04, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment