Mkuu wa Wilaya ya
Arusha ametoa angalizo kwa wananchi wote kuhusu tahadhari ya mlipuko wa ugonjwa
wa kipindupindu ambao umeripotiwa kuwepo katika Mikoa mbalimbali na maeneo ya
jirani na Wilaya hii.
Akizungumza
kwenye kikao maalumu na watendaji wa Kata, Maafisa Afya pamoja na wadau wa Afya
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.
Alexander Mnyeti ameelezea hatua ambazo Serikali ya Wilaya imechukua hadi
hivi sasa kudhibiti mlipuko wa ugonjwa kuwa ni:
-
Kuandaa
kambi maalumu kwa ajili ya wagonjwa watakaojitokeza –ipo katika Kituo cha Afya
Levolosi
-
Kuagiza
dawa na vifaa tiba kwa ajili ya tahadhari ya ugonjwa
-
Kusambaza mabango, vipeperushi na miongozo katika vituo vua kutolea huduma za afya,
Ofisi za Kata na mitaa pamoja na maeneo ya mikusanyiko
-
Kufanya
kikao na wadau wote na kuunda timu ya usimamizi wa mlipuko wa kipindupindu.
Kupitia kikao hiki kwa kauli moja wajumbe
walikubaliana hatua za kuchukua ili kupambana na mlipuko:
-
Kuhakikisha
upatikanaji wa maji safi kwenye maeneo
yote yenye uhaba wa maji
-
Kuchukua
Sampuli za maji katika Kata za pembezoni
-
Kupiga
marufuku uuzaji wa matunda yaliyomenywa,vyakula barabarani na pombe za kienyeji
-
Kutembelea
kaya na kukagua uwepo wa vyoo na matumizi yake
-
Kugawa
vidonge vya Kutibu maji kwenye kila Kaya
-
Kuwachukulia
hatua wote watakaokiuka wa kanuni za Afya
Pia
wananchi walishauriwa kujikinga na ugonjwa huu kwa njia zifuatazo;
-
Kunywa
maji yaliyochemchwa au yaliyowekewa dawa ya kuua vimelea
-
Kula
chakula cha moto kilichotayarishwa katika hali ya Usafi.
-
Kunawa
mikono kwa sabuni na maji ya kutitirika (usinawe ndani ya chombo).
-
Kuhakikisha
matumizi bora ya choo na kinyesi cha watoto wadogo kitupwe chooni
-
Kuepuka
kula matunda bila kuyaosha na kunywa juisi na vyakula vinavyouzwa kiholela.
TAHADHARI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 21, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment