Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo akiwasalimiana na viongozi
wa Wilaya katika eneo la mapokezi wakati
wa ziara yake Wilayani hapo.
|
Meneja wa Ranch hiyo Ndg.
Fidelis Ole Kashe akiwasilisha taarifa ya
Shamba hilo kwenye Kikao maalum na Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na
viongozi wa Wilaya
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akitoa maelekezo ya kubadilisha Hati ya
Umiliki wa shamba kutoka kwa TLCT kwenda kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei
na Ortukai.
|
Mbunge wa LongIDO Mhe.
Julius Kalanga(kulia) akiwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika ziara
ya Mkuu wa Mkoa.
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo akikagua Boma la Ngombe lililopo katika shamba la Manyara
Ranch.
|
Rc Gambo alitoa agizo hilo katika mikutano
ya hadhara iliyofanyika katika kata ya Elesilalei na Makuyuni baada ya
kutembelea miradi ya mamilioni ya fedha iliyopo ndani ya shamba hilo
inayofadhiliwa na African Wildlife Foundation{AWF} na kuelezwa kero na
changamoto zilizopo juu ya umiliki wa shamba hilo kwa taasisi ya TLCT.
Alisema nyaraka zinaonyesha
wazi kuwa Shamba hilo lilitolewa kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei na
Ortukai na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu mwaka 1999 kwa
ajili ya kilimo na ufugaji lakini hilo halikufanyika badala yake taasisi ya TLCT ikajimilikisha shamba hilo
kinyume na maagizo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kutokana na hali hiyo ninawaagiza
viongozi wote wa wilaya ya Monduli wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na
baraza la madiwani kuhakikisha ndani ya muda mfupi wanabadilisha umilikiwa wa
shamba hilo kutoka taasisi hiyo kwenda katika vijiji hivyo.
Gambo alisema serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli iko madarakani kwa
ajili ya kuwahudumia wanyonge na watu wa hali ya chini na kamwe haiwezi kuona
baadhi ya watu fulani wananufaika na rasilimali ya nchi kwa manufaa yao.
Alisema TLCT inamiliki shamba
hilo kinyume na maagizo kwani shamba hilo lilipaswa kumilikiwa na vijiji hivyo
kwa faida yao lakini walijitokeza wataalamu wakabadilisha maelekezo hayo na kujimilikisha kitu ambacho Serikali ya
Awamu ya Tano haiwezi kulivumilia kamwe.
‘’Nimeagiza umiliki wa shamba
hili unapaswa kubadilishwa haraka kwa kushirikisha vikao na kufuata taratibu
zote za kisheria ikiwemo kupitishwa na baraza la madiwani ili wananchi waweze
kunufaika na ardhi yao na sio watu wachache wanaolipwa mamilioni ya fedha bila
ya sababu za msingi’’alisema Gambo.
Naye Mbunge wa Jimbo la
Monduli, Mhe. Julius Kalanga na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Isack
Joseph wote kwa pamoja waliunga mkono wazo la Mkuu wa Mkoa na kusema kuwa
watatoa ushirikiano wa dhati kuhakikisha umiliki wa shamba hilo unabadilishwa
na kwenda kwa vijiji hivyo.
Mkurugenzi wa TLCT Bonfance
Ngimojiro alipopewa nafasi ya kujieleza katika mikutano hiyo miwili alisema
kuwa taasisi hiyo inaongozwa na bodi ya wadhamini yenye wajumbe nane wakiongozwa
na Mbunge wa zamani wa Mondul, Mhe. Edward Lowassa kama mwenyekiti wa Bodi
hiyo.
Ngimonjiro alikiri kupata amri
ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kutoka katika taasisi hiyo kwenda kwa
wananchi wa vijiji hivyo viwili lakini yeye hawezi kujuwa ni kwa nini amri hiyo
hadi jana haikutekelezwa.
Mkurugenzi huyo alisema yeye
ni mwajiriwa tu ambaye hajalipwa mishahara kwa miaka zaidi ya minne sasa katika
taasisi hiyo hivyo hawezi kujuwa kwa undani zaidi kushindikana kutekelezwa kwa
amri hiyo kwani wakitafutwa wahusika wanaweza kuwa na majibu sahihi.
Naye Meneja wa AWF, Fidelis
Ole Kashe yeye alisema kuwa wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu
sana ndani ya shamba hilo pamoja na kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo
katika shamba hilo ikiwemo shule,zahanati ,ufugaji wa kisasa na machinjio.
Kashe alisema utulivu ndio
njia pekee itayofanya miradi iliyopo katika shamba hilo kuendelea vinginevyo
wafadhili hao wanaweza kusikitisha kila kitu.
Alisema AWF imekuwa mstari wa
mbele kufadhili miradi mbalimbali katika wilaya ya Monduli na nchini kwa ujumla
na inapenda kuona fedha inazotoa zinafanya kazi iliyokusudiwa na sio
vinginevyo.
RC GAMBO AAGIZA MANYARA RANCHI IREJESHWE KWA WANANCHI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 21, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment