Mstahiki
Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti
Lazaro Bukhay(kulia) akipokea bendera ya Lions Club toka kwa Gavana Vinie Tinkumanya(kushoto), walipokuja
kukabidhi msaada katika Jiji la Arusha.
|
Add caption |
Mstahiki
Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro
Bukhay akikabidhiwa mashine za kusomea kwa wanafunzi wenye uoni hafifu
(Magnifier Machine) toka kwa wanachama wa Arusha City Lions Club.
|
Mstahiki
Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro
Bukhay akionyeshwa jinsi mashine za kusomea kwa wanafunzi wenye uoni hafifu
zinavyofanya kazi.
|
Mstahiki
Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro(tatu
kulia) akiwa na Diwani Mhe. Kinabo(anayefuata) pamoja na wanachama wa Arusha
City Lions Club walipokuja kukabidi msaada wa mashine za kusomea.
|
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro Bukhay amepokea msaada wa mashine mbili za
kusomea kwa wanafunzi wenye uoni hafifu (Magnifier Machine) zenye thamani zaidi
ya Tsh Mil 10 toka kwa wanachama wa Lions Club “Arusha City branch”.
Akipokea Msaada huo toka kwa Gavana Vinie Tinkumanya toka Uganda ambaye ni mwananchama wa Club aliyeongozana
na wanachama wa Arusha City Lions Club
alielezea furaha yake kupokea mashine hizo na kuwashru Club hiyo kwa kufikiria
na kukumbuka kundi maalumu la wanafunzi wenye uoni hafifu (Low vision)
“Tumekuwa tukipokea misaada mingi lakini ni mara chache
sana wafadhili kuwambuka vijana wetu hawa, mmetoa msaada wenye thamani sana kwa
Jiji la Arusha na mmeonyesha upendo wa hali ya juu kwa watoto wetu”alisema Meya
Bukhay.
Aliongeza kuwa pamoja na shukrani hizi pia naomba
ikiwezekana mtupatie na misaada zaidi ya ajili ya Elimu maalumu kwa kuwa tuna
mahitaji makubwa kwa ajili ya kukamilisha mahitaji ya watoto wetu wa Elimu
maalumu.
Naye Gavana
Tinkumanya alisema kutoa misaada ndio nguzo ya Club yao na wanapenda
kuwafikia watu wengi zaidi kwa kugusa maisha yao na kuwawezesha kupitia misaada
mbalimbali ya kijamii, Kielimu hata kiuchumi.
MEYA WA JIJI APOKEA MSAADA TOKA LIONS CLUB – ARUSHA CITY BRANCH
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 21, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment