Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook, pmchungaji aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua waduduinayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi.
Kampuni inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa hiyo watu , huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika kuwasilisha malalamiko.
Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho, akiiambia BBC kuwa anatumia mbinu zisizo za kawaida kuwaponya watu.
Nchi hiyo imekuwa na wimbila visa
ambapo wajumbe wa kanisawamekuwa wakitendewa vitendo visivyo vya kawaida ili
kupata tiba.
Katika picha zilizosambazwa kwenye
kurasa za Facebook na Twitter, Bwana Rabalago, anayeendesha kanisa la Mountzion
General Assembly katika jimbo la Limpopo, anaeonekana akimpulizia dawa ya
kuuwawadudu moja kwa moja kwenye macho yake na maeneo mengine mbali mbali ya
mwili mbele ya waumini wa kanisa lake.
'Nguvu
za Mungu'
Amemueleza mwandishi wa BBC Nomsa
Maseko aliyeko mjini Johannesburg kwamba alipuliza dawa hiyo kwenye uso wa
mmoja wa wanawake kwasababu alikuwa na maambukizi ya macho na kudai kuwa
"yuko sawa kwasababu anaamini nguvu za Mungu".
Pia alidai kuwa dawa hiyo ya Doom
inaweza kuponesha saratani na virusi vya HIV vinavyosababisha.
Kampuni inayotengeneza dawa ya Doom
kwa nembo ya Tiger inasema kuwa inamsihi s mchungaji aliyejitangazia kuwa
''nabii'' huko Limpopo - Lethebo Rabalogo kuacha kuwapuliza dawa ya wadudu
kwenye nyuso za binadamu kama sehemu ya imani ya kuabudu:
''Tunaona
tendo hili kuwa kutia hofu kubwa , na tungependa kubainisha wazi kwamba ni
hatari kupulizia Doom ama dawa nyingine yoyote ile ya wadudu kwenye macho ya
watu''.''Doom ilitengenezwa kwa ajili ya kuwauwa wadudu wa aina fulani ambao wameonyeshwa kwenye kopo, na maelezo yaliyoandikwa bayana kwenye kopo la Doom yameonya juu hatari na yanapaswa kufuatwa.''
''Kampuni ya Tiger iko katika mchakato wa kuwasiliana na Nabii kumtaka aache kufanya tendo hilo,'' imesema kampuni ya Tiger.
Mchungaji apulizia waumini Doom Afrika Kusini akidai ni tiba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 21, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment