Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,
Godbless Lema, amesafirishwa kutoka Mkoani Dodoma usiku wa kumkia jana na
kuswekwa kwa mara nyingine tena Mahabusu Mkoani Arusha kwa mahojiano ya kutoa
lugha za uchochezi.
Akizungumza leo na waandishi wa
habari ofisini kwake , Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo, amesema
Lema wamemweka mahabusu mpaka watakapomaliza mahojiano.
Amesema kuwa endapo watamaliza
mahojiano atafikishwa mahakamani wakati wowote, ili kujibu makosa anayokabiliwa
nayo.
Mkumbo amesema Lema amekuwa akitoa
maneno na lugha za uchochezi na kuzirudia kila mara, hivyo wameona vema wamweke
ndani.
Amesema juzi walimkamata na
kumuhoji, kisha kumwachia kwa dhamana, lakini kuna baadhi ya makosa hakuhojiwa,
na ndiyo wanamuhoji.
Aidha licha ya kumkamata Lema na
kuendelea kumuhoji, lakini hakutaja maneno yapi na lugha za uchochezi alizotoa
Mbunge huyo.
Novemba Mosi mwaka huu, Kamanda
Mkumbo akiwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, alitaja maneno
ya uchochezi anayodaiwa Lema kutaja kuwa ni: “Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania akiendelea kukandamiza demokrasia,siasa za ukandamizaji
taifa litaingia katika umwagaji wa damu,nchi hii inaandaliwa kwenda katika
utawala wa kidikteta,”
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema aswekwa mahabusu kwa mahojiano zaidi.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 04, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 04, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment