KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe jana alisababisha taharuki katika kikao cha Bunge baada
ya kuzusha tuhuma za rushwa kwa wabunge wa CCM katika kipindi cha maswali na majibu
na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Ingawa swali lake hilo lenye
tuhuma lilizuiwa kujibiwa na Naibu Spika, Dk Tulia Akson kwa kuwa halikuwa
swali la kisera, hoja iliibuliwa tena na wabunge wengine wakati wa kuingia
kipindi cha majadiliano, kama miongozo.
Mbowe katika swali lake kwa Waziri Mkuu alituhumu wabunge wa CCM, kupewa rushwa ya Sh milioni 10 kila mmoja na serikali ya chama hicho ili kuupitisha Muswada wa Huduma za Habari unaowasilishwa bungeni leo.
Aidha alidai rushwa hiyo, pia imetolewa kupitisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18. Pamoja na tuhuma hizo kutojibiwa na Waziri Mkuu kutokana na muundo wa maswali ya papo kwa hapo kugusa sera, Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema) aliomba mwongozo wa Spika huku akitaka kuundwe Tume Huru ya Kimahakama ya Bunge, kuchunguza tuhuma hizo.
Naye Mbunge wa Chemba, Juma
Nkamia (CCM) alisimama na kuomba mwongozo, na kumtaka Mbowe athibitishe tuhuma
hizo au achukuliwe hatua.
Nkamia alisema yeye akiwa Mbunge wa CCM, hajapata rushwa hiyo wala hakuiona na kuhoji kwa nini Mbowe ahoji wakati yeye si Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), hivyo akitaka Mbowe athibitishe tuhuma hizo na akishindwa, alitaka mwongozo ni hatua gani Bunge itamchukulia.
MILIONI 10 NI KWELI MH WAZIRI SWALI LA MBOWE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 04, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 04, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment