LEMA AENDELEA KUKAA RUMANDE BAADA YA KUKOSA DHAMANA




Harakati za kumpatia dhamana mbunge wa Arusha Mh Godbless Lema anayekabiliwa na kesi ya uchochezi zimeendelea kugonga ukuta baada mahakama kuu kanda ya Arusha kusikiliza hoja za pande zote na kuahidi kuzitolea uamuzi baada ya siku tano

Hatua hiyo imekuja baada ya mawakili wa pande zote kuwasilisha hoja zao kila upande ukitetea hoja yake mbele ya jaji wa mahakama hiyo Sekela Moshi aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo.

Jopo la mawakili wanaomtetea Mh Lema wakiongozwa na wakili msomi Peter Kibatala, John Malya, Adamu Jabiri, Sheki Mfinanga na Charles Adirian Faraji Mangula walimweleza Mh jaji Sekela Moshi kuwa taratibu za kuweka pingamizi zilikiukwa hivyo shauri hilo litupiliwe mbali na mteja wao apewe dhamana

Kwa upande wa mawakili wa serikali walioongozwa na wakili msomi Paul Kadushi na Mosese Marandu waliendelea kushikilia na kutetea hoja yao kuwa mtuhumiwa hastahili kupewa dhamana kwa sababu ambazo walishaziwasilisha na kwamba pingamizi waliloweka linakubalika kisheria na kama mtumiwa anaona kuwa lina mapungufu anapashwa kukata rufaa na sio kuwasilisha barua kama alivyofanya

ya mvutano wa mjadala mkali wa kisheria wa mawakili hao wa pande mbili Mh jaji Sekela Moshi akaiambia mahakama kuwa kulingana na uzito wa hoja anahitaji muda wa kuzipitia na kwamba atatoa maamuzi siku ya jumanne tarehe 22 .11.2016

maamuzi hayo mtuhumiwa Lema alirudishwa tena mahabusu kusubiri siku ya tarehe 21.11.2016 atakapopandishwa kizimbani tena kuendelea na kesi yake ya msingi ya uchochezi na maneno ya kashifa
LEMA AENDELEA KUKAA RUMANDE BAADA YA KUKOSA DHAMANA LEMA AENDELEA KUKAA RUMANDE BAADA YA KUKOSA DHAMANA Reviewed by KUSAGANEWS on November 17, 2016 Rating: 5

No comments: