Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo(mbele kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa CWCD Bi. Hindu Ally Mbwego (kulia mbele)
pamoja na baadhi ya watoto wa Pamoja Tuwalee.
|
Mkurugenzi wa WEI-TANZANIA
Bi. Lilian Badi (aliyesimama)
akielezea mafanikio ya Mradi wakati wa Mkutano wa kuhitimisha mradi wa Pamoja
Tuwalee.
|
Mkurugenzi Mkuu wa World
Education Inc Bi.Gill Garb akitoa taaria ya utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee
kupitia WEI-Bantwana.
|
Mwakilishi wa US-AID
Tanzania Bi. Maria Busquets akielezea namna ambavyo Shirika lake
limefanikisha utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee.
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akizungumza na wadau wa Mkutano
|
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati)
akiwa na wataalam kutoka Halmashauri ya
Korogwe waliofanikisha utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee.
|
NTEGHENJWA
HOSSEAH - ARUSHA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amewataka wafadhili na wadau wa watoto
kubuni miradi inayoendana na kusaidia
Mpango wa Serikali wa Elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari ili kupunguza changamoto zinazojitokeza kwa
sasa na kuuwezesha mpango huu kutekelezwa kwa mafanikio makubwa.
Mhe. Gambo ameyasema
hayo wakati wa Mkutano wa kushirikishana tuliojifunza wakati wa utekelezaji wa
mpango wa pamoja tuwalee uliotekelezwa kwa miaka sita kwenye Kanda ya
Kaskazini na ambao kwa sasa umemaliza
muda wake ulifanyika kwenye Hotel ya Mt Meru Jijini hapa.
Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa
amesema kazi kubwa imefanyika wakati utekelezaji wote wa mradi na mafanikio yake tumeonekana kwani watoto wamefikiwa
na kusaidiwa kutoka katika mazingira hatarishi yaliyokuwa yanawakabili na
wengine kupatiwa kadi za msamaha wa matibabu na zaidi mradi huu umekabidhiwa
kwa Halmashauri husika ambazo
zitaendelea kusimamia na kutekeleza
mipango iliyowekwa chini ya mradi wa Pamoja Tuwalee.
Aliendelea kusema kuwa kukamilika kwa mradi
huu katika awamu ya kwanza ni wazi kabisa kwamba ni maandalizi ya mradi
mwingine ambao utakua na malengo yanayoshabihiana na programu ya awali hivyo ni
vyema kwa kuwa walengwa bado ni watoto niwatake wadau kubuni miradi utakaolenga
kusaidia Elimu bure na kwa kuwa watoto wote wanapata Elimu bure kupitia mpango
huu basi ni vyema mkaelekeza nguvu kwenye utoaji wa Chakula kwa wananfunzi
suala ambalo tumeona ni changamoto kwa watoto wetu.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la WEI – Bantwana “World Education
Inc” Bi. Gill Gap alisema
wanajivunia kuwa Taasisi iliyofanikisha utekelezaji wa mradi wa pamoja kwa
ushirkiano wa Serikali ya Tanzania katia utekelezaji wa mradi pamoja na
Serikali ya Marekani kwa ufadhili mradi huu. Pamoja Tuwalee ilikuwa maalumu
kuwalinda watoto walio katika mazingira hatarishi na kutoa Elimu kwa wazazi walioathirika namna
ya kuishi na watoto hao pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa Halmashauri
kuendeleleza jitahada za mradi huu.
Jacklin Badi ni
Mkurugenzi wa WEI – Tanzania anasema “Bantwana ni kitengo ndani ya Shirika la WEI kinachohudumia watoto na hapa
Tanzania tulianza utekelezaji mwaka 2010
na mpaka sasa tumefanikiwa kuwafikia watoto 1,470,445 pamoja na wazazi wao na
wameweza kupatiwa huduma jumuishi za
kuwasaidia na kuwalinda watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya
Wanawake, watoto na vijana “Center for women, Children and Youth Development (CWCD)
Bi. Hindu Ally Mbwego ambao ni
watekelezaji wa mradi huu wa Pamoja Tuwalee kupitia mwamvuli wa WEI-Bantwana
amesema wamefanikiwa kuwafika katika maeneo yote ya Jiji la Arusha, Halmashauri
ya Karatu na Moshi na wanajivunia mafanikio
waliyoyapata kutokana na mradi huu.
Tumebadilisha maisha ya watoto na kuhakikisha
usalama wao katika Jamii wanazoishi, tumewatambua wazazi wenye watoto
walioathirika na kuwapa elimu ya jinsi ya kuwafahamisha watoto wenye hali hiyo
na namna ya kuishi nao ili waweze kukua katika malezi bora na afya njema
sanjari na kupata Elimu alisema Bi.
Hindu.
Mradi wa pamoja Tuwalee ni mpango wa Kitaifa
wa miaka mitano uliotekelezwa na fedha za mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa
kupunguza makali ya virusi vya ukimwi kwa waathirka kupitia Shirika la Misaada
la Marekani la USAID na kutekelezwa na
WEI-Bantwana pamoja na Kituo cha maendeleo ya Wanawake, watoto na vijana
kilichopo Jijini Arusha.
MHE. GAMBO AWATAKA WAFADHILI KUTOA CHAKULA MASHULENI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 17, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment