WATU 77 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA AJALI ZA BARABARANI KUANZIA SEPTEMBA 26 MWAKA HUU MKOANI KAGERA



Jumla ya watu 77 walipoteza maisha katika mkoa wa Kagera kutokana na matukio ya ajali za barabarani 79 zilizotokea mkoani humo katika kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi Septemba mwaka huu zilizosababishwa na waendesha magari na pikipiki.

Hayo yameelezwa na mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi, William Mkonda ambaye mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera wakati wa kufunga wiki ya nenda kwa usalama wilayani ngara iliyoandaliwa na mkoa wa Kagera kuanzia Septemba 26, mwaka huu, 

Akizungumza wakati akielezea mambo yanayosababisha ajali katika mkoa huo, amesema kwa sasa ajali zimepungua kwa kuwa mwaka jana katika kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi Septemba jumla ya watu 81 walipoteza maisha kutokana na ajali 102 za magari na pikipiki.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani ya mkoa wa Kagera, Winston Kabanteba ameeelezea shughuli mbalimbali zilizofanyika katika wiki ya nenda kwa usalama, akizungumza amesema katika wiki hiyo 

Elimu ya masuala ya usalama barabarani imetolewa kwa waendesha pikipiki na wanafunzi ambao wanasoma kwenye shule zilizoko kando ya barabara, naye mkuu wa wilaya ya ngara,Luteni Kanali Michael Mntenjele amewataka waendesha vyombo vya moto kwa kuzingatia kauli mbiu ya jeshi la polisi ya kutii sheria bila shuruti.

WATU 77 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA AJALI ZA BARABARANI KUANZIA SEPTEMBA 26 MWAKA HUU MKOANI KAGERA WATU 77 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA AJALI ZA BARABARANI KUANZIA SEPTEMBA 26 MWAKA HUU MKOANI KAGERA Reviewed by KUSAGANEWS on October 09, 2016 Rating: 5

No comments: