KIONGOZI wa chama cha ACT–Wazalendo, Zitto Kabwe,
amemshauri Rais John Magufuli, kuwafikisha kwenye vyombo vya nidhamu na sheria
wote aliowatumbua tangu alipoingia madarakani.
Alisema watu hao waliotumbuliwa kuanzia mwaka jana
hadi Agosti mwaka huu, ambao idadi yao ni takribani 130, wafikishwe kwenye
vyombo vya kisheria na nidhamu ili viwaeleze Watanzania kuhusu kile
wanachotuhumiwa nacho watumishi hao.
Halikadhalika alimshauri Rais Magufuli kufuata misingi ya haki na usawa katika kuwachukulia hatua baadhi ya watumishi wa umma aliowatumbua kwa tuhuma mbalimbali.
Zitto aliyasema hayo jana Dar es Salaam katika mkutano mkuu wa ACT-Wazalendo, unaojadili mambo kadhaa yakiwamo, hali ya siasa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 pamoja na uzoefu wa kisiasa wa mataifa mengine ya Afrika.
ZITTO- JPM WAFIKISHE MAHAKAMANI ULIOWATUMBUA MAJIPU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 09, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 09, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment