Taarifa kutoka Ikulu: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mhandisi James Mitayakingi Kilaba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi James Mitayakingi Kilaba umeanza jana Jumamosi tarehe 08 Oktoba, 2016.
Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba alikuwa akikaimu nafasi hiyo, baada ya uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba kutenguliwa.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
09 Oktoba, 2016Source
Taarifa kutoka Ikulu: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCR
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 09, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 09, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment