WATU 2 WAWILI WANUSURIKA NA AJALI YA BASI LA KAMPUNI YA HOOD



Basi la Kampuni ya HOOD likiwa limeingia katika nyumba ya biashara baada ya kupoteza muelekeo
basi la Hood likiwa ndani ya nyumba baada ya kupioteza muelekeo

Wananchi wakishuhudia ajali maeneo ya kona nairobi
Watu wawili wamenusurika kifo akiwemo dereva wa Basi la kampuni ya hood lenye namba za usajli T 484 AXV pamoja na muhudumu wa nyumba moja ya biashara iliyopo mtaa wa tindigani kata ya ungalimited; kufuatia basi hilo kufeli breki na kupoteza na kisha kuigonga nyumba hiyo.

Muhudumu wa nyumba hiyo Robina Marwa amesema ajali hiyo imetokea majira saa tisa usiku wa kuamkia leo wakati akifanya usafi ili afunge biashara lakini gafla alisikia kishindo kikubwa na kuona basi hilo likigonga nyumba hiyo na kuingia ndani.

Amesema basi hilo lilikuwa likitokea barabara ya Tekniko na lilipofika eneo la kona na Nairobi lilipoteza mwelekeo na kisha kuigonga nyumba hiyo ya biashara ambapo aliejeruhiwa sehemu ya mkono pamoja na kuharibu eneo la mbele la ukuta wa nyumba hiyo,milango, madirisha,viti,pamoja meza moja ya pool Table.

Mmliki wa nyumba hiyo Chola Mollel amesema bado anaendelea kufanya tadhmini ya mali zilizoharibika ili kujua dhamani yake.  
WATU 2 WAWILI WANUSURIKA NA AJALI YA BASI LA KAMPUNI YA HOOD WATU 2 WAWILI WANUSURIKA NA  AJALI YA BASI LA KAMPUNI YA HOOD Reviewed by KUSAGANEWS on October 27, 2016 Rating: 5

No comments: