WANAFUNZI 11 WATUHUMIWA KUJIHUSISHA KIMAPENZI NA MBWA ARUSHA



Wanafunzi 11 wa kiume katika shule ya msingi Sombetini jijini Arusha wanatuhumiwa kufanya ngono na mbwa eneo la mto Ngarenaro  kata ya ngaranaro jijini arusha na kwamba watoto hao ni wa miaka kati ya miaka saba na 11 wa darasa la tatu.

Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha , Charles Mkumbo amesema jeshi la polisi haliwezi kuwafungulia kesi wanafunzi hao ambao wamekiri kufanya vitendo hivyo mara kadhaa, kutokana na umri wao kuwa mdogo. 

Kamanda mkumbo amesema Kisheria, ili mtu aweze kushitakiwa na kosa hilo anapaswa awe mtu mzima kuanzia miaka 13 na kuendelea na mtoto wa miaka 10 na kurudi nyuma kisheria hastahili kushtakiwa kwa jambo lolote alilolitenda la kijinai.

Aidha amesema jeshi hilo linawatafuta vijana waliowafundisha kufanya mapenzi na mbwa wakati watoto hao wakiendelea kupata ushauri wa kitaalamu.

Pamoja na hayo ameagiza timu yake ya wataalamu wa dawati la jinsia kufika shlue ya msingi sombetini kwa ajili ya kutoa ushauri kwa watoto ili kuepukana na vitendo hivyo ambavyo siyo vizuri kwa jamii na taifa kwa ujumla.
WANAFUNZI 11 WATUHUMIWA KUJIHUSISHA KIMAPENZI NA MBWA ARUSHA WANAFUNZI 11 WATUHUMIWA KUJIHUSISHA KIMAPENZI NA MBWA ARUSHA Reviewed by KUSAGANEWS on October 27, 2016 Rating: 5

No comments: