RC PAUL MAKONDA AZITAJA SABABU ZA UJIO WA MFALME WA MOROCO KWA TAIFA



Tanzania inataraji kumpokea Mfalme wa Moroco Mohammed VI  akiambatana na msafara wa watu wapatao 1000 Mfalme huyo anatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 23 mwaka huu katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Mbali na ujio huo kwa mara ya kwanza nchi ya itaweka historia ya kuwasili ndege sita kubwa aina ya Boil na ndege ndogo mbili kwa ajili ya shughuli za utalii, na kuhitimisha ziara hiyo Octoba 27.
Akizungumza Jijini  Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda amesema Rais John Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wawekezaji wanakuja nchini kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi na kuitangaza kimataifa zaidi ambapo amesema ujio wa wageni huo utasaidia kwa kiasi kikubwa nchi kuingiza mapato katika suala zima la utalii na uchiumi.

Huku akiongeza kuwa pamoja na mambo mengine Mfalme Mohamed VI anatarajiwa kusaini mikataba ya kimakubaliano 11 akiwa na Mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli yenye tija kwa Taifa ikiwemo katika masuala ya kilimo kwa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo pembejeo za kilimo, masuala ya mifugo na uvuvi, nishati na madini, masuala ya utalii ambapo kuna ndege mbili za ugeni huo zitatumika kwa ajili ya utalii pekee, pia ujio huo utadumisha ushirikiano wa kisiasa na kushirikiana kwa Wizara za Mambo ya nje za Moroco na Tanzania.

 

RC PAUL MAKONDA AZITAJA SABABU ZA UJIO WA MFALME WA MOROCO KWA TAIFA RC PAUL  MAKONDA AZITAJA SABABU  ZA UJIO WA MFALME WA MOROCO KWA TAIFA Reviewed by KUSAGANEWS on October 21, 2016 Rating: 5

No comments: