MKOA WA ARUSHA NI ZAIDI YA ARUSHA MJINI ASEMA OLENASHA



NAIBU Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole Nasha amesema kuwa baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Arusha hazina mgogoro wa kiongozi baina yao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha badala yake amemtaka Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro na Mbunge wa Arusha Mjini, God bless Lema kutafuta njia nyingine za kutatua changamoto yao.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya  Arumeru, Alexander Mnyeti amesema kuwa ameandika barua kwa Rais John Magufuli ili kutoa kibali cha kufuta mashamba 12 yaliyopo wilayani hapo ili yaweze kugaiwa kwa wananchi kwa sababu hayaendelezwi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye ukumbi wa mikutano uliopo jengo la mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), Ole mmikNasha amesema si busara kwa viongozi hao ambao ni mbunge na meya kusema kuwa Arusha kunamgogoro wa kiuongozi na Mkuu wa mkoa Gambo badala yake watafute mbinu za kutatua mgogoro huo kwani Arusha inawilaya nyingi na miongoni mwa wilaya hizo hazina mgogoro wa kiuongozi au kiutawala na Gambo.

Amesema Arusha ni kubwa na hoja ya kiuongozi ni ya kwao na si ya kikao kizima hivyo akaomba watambue kuwa Arusha ni zaidi ya Arusha mjini hivyo wajadili hoja za migogoro ya ardhi ambazo ndiyo agenda ya kikao hicho na hoja ya mbunge na Meya wa jiji watafute siku nyingine au waiweke kwenye mengineyo.

Hoja hiyo ya meya Lazaro aliibua mwanzoni kwenye kikao hicho kwa kusema kuwa kwanini halmashauri ya Jiji la Arusha itumie fedha za halmashauri hiyo kugharamia posho za kikao hicho na kuongeza kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma pia amesisitiza Arusha kunamgogoro wa kiutendaji kati ya Mkuu wa mkoa na wao kama madiwani lakini pia yeye kama Meya wa Jiji hilo hashirikishwi kwenye ziara za viongozi wa serikali pamoja na ziara za mkuu wa mkoa kwenye kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Naye mbunge lema amemsihi aliyekuwa Mwenyekiti wa muda wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta kuwa ajenda hiyo iwekwe mapema ili mkuu wa mkoa atakapofika kwenye kikao hicho aikute na waijadili hali ambayo iliibua mikono kwa wajumbe mbalimbali na ndipo hapo Naibu Waziri Nasha alipomaliza kwa kusisitiza kuwa Arusha ni zaidi ya Arusha mjini.

Baada ya muda Mkuu wa mkoa alifika na kuendesha kikao hicho ambapo kila Mkuu wa Wilaya alisimama na kueleza changamoto na utatuzi wa migogoro ya ardhi kwenye Wilaya zao ambapo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti amesema Wilaya ya Arumeru ni mojawapo kati ya Wilaya zenye changamoto kubwa ya ardhi ambapo hivi sasa amemwandikia barua Rais Mafuguli kwaajili ya kufuta mshamba 12 yaliyopo Wilayani Arumeru.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo amesema wilaya yake inajitahidi kutatua changamoto za ardhi na kutoa rai kwa serikali kupitia Wizara y Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuwasaidia ili kutatua mgogoro wa shamba la Barakwai lililopo mpakani mwa Wilaya ya Longido na Siha kuhusu mgogoro wa mpaka na malisho.

Naye Mkuu wa mkoa alimuomba mbunge wa Monduli, Julius Kalanga kusubiri serikali ichunguze chanzo cha mgogoro wa shamba la Stein lililopo eneo la Makuyuni Wilayani humo ili kubaini shamba hilo ambalo mwekezaji alitoa eka 3000 kwa ajili ya wananchi ni kweli zilienda kwa wananchi au watu walitumia mwamvuli wa shamba hilo kwaajili ya kujimilikisha ardhi hiyo.

Pia Gambo ametoa angalizo kwa wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi baina y vijiji na vijiji badala ya migogoro hiyo kuletwa kwake na mkuu wa wilaya atakayeshindwa kutatua migogoro hiyo ikimfikia mezani kwake atalishughulikia ikiwemo dc huyo kuondoka na barua ya kushindwa kutatua changamoto za wilaya yake.
MKOA WA ARUSHA NI ZAIDI YA ARUSHA MJINI ASEMA OLENASHA MKOA WA ARUSHA NI ZAIDI YA ARUSHA MJINI ASEMA OLENASHA Reviewed by KUSAGANEWS on October 21, 2016 Rating: 5

No comments: