![]() |
| Mkurugenzi wa Idara ya Habari Hassan Abbas |
Aidha, amesema kuwa sheria hiyo itahusu vyombo vya habari vya mfumo wa
machapisho, ambavyo ni pamoja na magazeti na majarida na si mitandao ya kijamii
kama wadau wanatafsiri.
WANATASNIA ya habari nchini wametakiwa kuukubali muswada wa sheria wa
huduma ya habari unaotarajia kuwasilishwa hivi karibuni Bungeni kwa kuwa
umekusudia kuifanya taaluma hiyo kuaminika kwa jamii.
Hayo yamasemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Hassan Abbas Jijini Dar
es salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari vilivyopo Jijini
humo.
Alisema kwa muda mrefu wadau wa Habari na wanatasnia wenyewe wamekuwa na
kiu ya kupata sheria mpya baada ya ile ya mwaka 1976, ambayo imepitwa na
wakati.
“Kutokana na teknolojia kubadilika, ni wakati mwafaka wa kuanzishwa kwa
taasisi inayosimamia maadili ya wanahabari, hivyo vyombo vya Habari waliona ni
muhimu kuwa na sheria mpya itakayokidhi mabadiliko hayo” alisema Abbas.
Aidha, alisema kuwa sheria hiyo itahusu vyombo vya habari vya mfumo wa
machapisho, ambavyo ni pamoja na magazeti na majarida na si mitandao ya kijamii
kama wadau wanatafsiri.
Aliongeza kuwa miongoni mwa masuala yanayozungumziwa katika muswada huo
ni pamoja na kuundwa kwa bodi ya ithibati kwa wanahabari, Baraza huru la
habari, Ofisi ya mkurugenzi wa habari, na Mfuko wa mafunzo kwa wanahabari.
Abbas aliongeza Serikali imewashirikisha wadau muhimu wakati wa mchakato
wa kuandaa muswada huo ikiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha
wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na
baadhi ya wadau wa haki za binadamu.
Aidha alitoa wito kwa wadau wote kutoa maoni yao kwa lengo la kuboresha
muswada huo sheria kupitia barua pepe ya ofisi ya Bunge can.bunge.go.tz ili
kuyawasilisha mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za maendeleo ya
jamii.
MUSWADA WA SHERIA ZA HABARI UTAIPA TASNIA HESHIMA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 26, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 26, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment